Mayweather Kulipia Mazishi ya George Floyd

Bondia Floyd Mayweather ameomba kulipia mazishi ya Mmarekani mweusi aliyeuawa akiwa mikononi mwa polisi George Floyd.

Kifo cha George Floyd kimeigusa jamii kubwa ya Waafrika weusi, wanamichezo na wanaharakati wengi wa masuala ya ubaguzi wa rangi na kupelekea maandamano kule Minneapolis ambako kifo hiki kilitokea.

Floydalikamatwa na polisi  wanne kwa kuhisiwa kughushi bili na kisha akakandamizwa kwa goti shingoni na askari aliyeitwa Derek Chauvin kwa zaidi ya dakika 10 akiwa analalamika kuwa “Nashindwa kupumua” na askari aliyekuwa akimkandamiza akapuuzia, ikitajwa kuwa ndiyo sababu ya kifo chake.

Si kifo cha kwanza cha Mmarekani mweusi kinachohusiswa na ubaguzi. Wanamichezo wengi weusi na wasio weusi na wanaharakati ambao wameguswa na kifo cha George wametoa yaliyo ya moyoni na kutoa wito wa mauaji ya aina hii yanayohusiana na ubaguzi wa rangi yanayotekelezwa polisi au raia wa kawaida kufika mwisho.

Floyd Mayweather alitangaza kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter kuwa ameta ofa ya kugaharamia mazishi ya George kwa familia yake. Vyanzo kadhaa pia vimethibisha kuwa familia imekubali ofa hiyo.

Polisi amabaye alihusika na kifo cha Floyd tayari anaripotiwa kuwa amefutwa kazi na anashikiliwa kwa makosa ya daraja la tatu na daraja la pili ya uuaji. Askari wengine watatu waliohusika wakati wa ukamataji hawajafunguliwa mashtaka.

46 Komentara

    Mungu akubariki sana Mayweather akuongozee ulipo toa,,na marehemu apumzike kwa aman

    Jibu

    Kifo cha mtu mweusi marekani kimeamsha hisia za wengi mno na mayweather kujitolea kwa gharama hizo ni kuonyesha hisia zake kwa wajina mwenzake

    Jibu

    Ni watu wenye moyo kama huo mungu ambariki sana ampe hitaji la moyo wake kama unavyo hitajika

    Jibu

    Mayweather mungu atakulipa
    Na uzidi kuwa na moyo huo

    Jibu

    Inauma sana ila ndio ishakuwa hivyo,pumzika kwa amani mweusi mwenzangu Amina🙏🙏

    Jibu

    Mungu akuongezee pale utakapotoa maywearther..

    Jibu

    Aisee ubarikiwe sana kwa hilo

    Jibu

    Hii inasikitika sana.laana nyingine ni za kujitakia

    Jibu

    Mayweather utabarikiwa

    Jibu

    Mungu ambariki

    Jibu

    Imeumiza kila mtu kwa Kweli #Meridianbettz

    Jibu

    Ubarkiwe

    Jibu

    Mungu atakulipa kwa moyo wako

    Jibu

    hongera Mayweather uendelee na moyo huo huo usiishie apo

    Jibu

    Kafanya jambo jema na LA kuigwa

    Jibu

    Abarikiwe

    Jibu

    Vizuri kijana,lazima tupendane mana tofauti ni rangi ila mtu mmoja.

    Jibu

    unamoyo wa pekee maywether mungu akubariki

    Jibu

    Walichokifanya askari wa Marekani sio jambo la kiungwana…Mungu atalipa kwa mywhether kwa upendo wake

    Jibu

    Hii inatafasirika kama kuguswa kwa hali ya juu ijapokuwa wachache wataibeba kama kujikweza ….so sad moment kwa wajina wake ….#Justice for Floyd

    Jibu

    Ubalikiwe sana

    Jibu

    Ni jambo zuri sana aliloamua kulifanya Mayweather kulipia mazishi ya George Floyd kwani mungu amzidishie kwa uungwana wake Mayweather

    Jibu

    Ni vizuri kudikisha ujumbe kwa wanajifanya kuwa dunia ni yao Ila ipo siku Mambo yatabadilika

    Jibu

    Safi Sana aendelee kua na moyo Kama huo

    Jibu

    Huyu jmaa kapata umaarufu baada ya kufa, maana familia yake ishapata pesa nying had sasa na zinaendelea

    Jibu

    Safii sana pongezi kwake mwamba Mayweather mungu abaliki

    Jibu

    So sad..hongera Mayweather

    Jibu

    Mayweather ameonyesha moyo kwel kwa hili Jambo inafaa kuigwa

    Jibu

    Duh Suala George Floyd limeleta tafurani duniani, Mayweather ameona hiyo ndio namna ya kuonyesha kuguswa kwake#meridianbettz

    Jibu

    Ongera mayweather..! Umewakilisha wa African

    Jibu

    Si kifo cha kwanza cha Mmarekani mweusi kinachohusiswa na ubaguzi vitendo ivi vimezid kuongezeka viongozi wanaitaji kujitasimini

    Jibu

    Mungu atawalipa wote waliohusika.inauma sana

    Jibu

    Jambo zuri alilolifanya Mungu atambariki kulingana na wema wake

    Jibu

    Kutoa ni moyo Wala si utajir

    Jibu

    Kifo chake kinasikitisha mungu akubariki maywether

    Jibu

    Ni jambo zuri sana kufanya hivyo maana anamuenzi kwa Hishima kubwa

    Jibu

    Habarikiwe sana

    Jibu

    Dah kifo Cha George kinaumiza sana

    Jibu

    huu ndio uungwana na umoja unaotakiwa, hiki ni kitu kibaya sana ila kwa kua ni mweusi litaishia hewani tuu bila hatua kubwa kuchukuliwa, HONGERA MAYWEATHER

    Jibu

    Swala la ubaguzi limekuwa likitunyima haki na fursa sana waafrika katika nchi za wenzetu, Sijui lini litafikia mwisho hili jambo, Its time for the whole world to stand as one

    Jibu

    so sad, his death arousal brutality feeling against police officers

    Jibu

    Ni huzuni ubaguzi cyo mzur ongera mayweather kwa kujitolea uko

    Jibu

    Abarikiwe sana

    Jibu

    Aisee mungu akubariki akuzishie pale ulipo papunguza

    Jibu

    Asante kwa ukaribu wa mwezi mungu hakubaliki.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.