Mbwana Samata Alizaliwa Awe Shujaa

Leo ukitaja jina la Mbwana ally Samata watu wengi wamelifahamu kupitia kipaji chake soka ambapo hadi sasa anaitangaza vizuri Tanzania kimataifa ambapo kwa sasa anakipiga katika timu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi kuu ya Nchini Uingereza..

Kama unakumbuka Septemba 5, 2018 kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha akiwa kwenye jezi ya Taifa Stars, picha hiyo iliambatana na ujumbe huu: “Muda mwingine Mungu hakupi unaloliomba ila anakupa linalokustahili. Kabla ya soka nilikuwa natamani kuwa mwanajeshi, je kwa sura hii unadhani ningependeza kuwa soja?

Kumbe bwana Samatta anatoka kwenye familia ya kipolisi!! Baba yake Mzee Ally Samatta na mama yake wote walikuwa ni askari wa Jeshi la Polisi Tanzania. Lakini hata babu yake Mbwana (Mzee Pazi Samatta) alikuwa askari polisi wa enzi hizo.

Haikuishia hapo, kaka zake wawili pia walifata mkondo huo ambapo mmoja ni askari wa Jeshi la Polisi Tanzania mwingine ni mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Kwa hiyo Samatta kuwa na ndoto za kuwa mwanajeshi huenda ilitokana na mazingira ya aina ya familia anayotoka.

Mzee Ally Samatta anasema kama Mbwana Samatta asingekuwa na kipaji kikubwa kwenye soka basi baada ya kumaliza elimu ya kidato cha nne huende angepelekwa kujiunga na Jeshi la Polisi kwa sababu isingekuwa kazi ngumu maana wazazi wote walikuwa askari polisi tena wenye vyeo. Suala la Samagoal kujiunga na jeshi la polisi lilikuwa ndani ya uwezo wao.

3 Komentara

    Jembe letu sakata,mwamba wa tanzania,hakika anapeperusha vyema bendera yetu ya Tanzania,samata oyeee

    Jibu

    Anaiwakilisha vema sana nchi yake

    Jibu

    Sama goal shujaa kweli

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.