Benjamin Mendy aliekua mchezaji wa Manchester City ameachiwa huru rasmi baada ya mahakama kutomkuta na hatia kupitia kesi zilizokua zinamkabili mchezaji huyo.

Mahakama ya Chester Court nchini Uingereza imethibitisha staa huyo hana hatia kupitia kesi ya unyanyasaji wa kingono ambapo alishtakiwa kwa kumbaka binti wa miaka 19 huko nyumbani kwake Prestbury,Chesire mwezi wa saba mwaka 2021 ambapo kitendo kilichomfanya mchezaji huyo kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kushtakiwa kuhusiana na kesi hiyo.

mendyMendy hakua mwenyewe katika kesi hiyo alikua na mshirika wake gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Louis Saha ambae nae alithumiwa pamoja mchezaji huyo huku nae mahakama ikimkuta hana hatia kupitia kesi hiyo.

Hivo mchezaji huyo ambaye alikua nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kwasasa ataruhusiwa kuendelea na shughuli zake kama ilivyokua mwanzo huku akisisitiza hatazingumza lolote kwa wakati huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa