Mathias De Ligt mchezaji wa klabu ya Fc Bayern Munich na timu ya taifa ya Uholanzi ameeleza anaamini hajakosea kundoka klabu ya Juventus majira haya ya joto.

Beki huyo raia wa Uholanzi ambaye tangu ahamie klabuni hapo timu haijafanya vizuri bado kwani imeshinda michezo mitatu tu ya awali na kusuluhu michezo minne lakini haimfanyi beki huyo kuamini amekwenda sehemu sahihi.

mathias de ligtDe ligt ameeleza klabu ya Juventus ni klabu kubwa na alifurahia wakati wake akiwa katika klabu hiyo lakini alifikiri umefika muda wa kutafuta changamoto sehemu nyingine aliliambia jarida moja wakati akiwa katika timu ya taifa.

“Juventus ni timu kubwa lakini kuja hapa ni hatua nyingine kwangu,kwasababu Bayern wana nia ya kushinda ligi ya mabingwa ulaya kitu ambacho sikua nakiona pale Juve”.

Beki huyo zao la Ajax ya nchini Uholanzi amesisitiza kuondoka kwake Juvetus na kuelekea Bayern ni sehemu ya ukuaji kwake, kwakua pia ana ndoto ya kushinda ligi ya mabingwa ulaya na anaona sehemu sahihi ya kupata ni kwa miamba hiyo ya soka nchini Ujerumani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa