Ndoto za watu wengi huanzia mbali sana tangia wakiwa wadogo. Lakini ni watu wachache sana ambao hiuziishi ndoto zao wanapokuwa watu wazima. Unafikiria kuhusu ndoto zako za utotoni na maisha unayoyaishi sasa, ni sawa? Usijali, haupo peke yako mhuhimu kufanikiwa. Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ni kati ya watu wanaoishi ndoto zao!
Rafikiye Jurgen Klopp, Jens Haas, anakumbuka sana kipaji cha meneja huyu tangu alipokuwa mdogo. Walikuwa na umri wa miaka 11 tu wakati alipoamini kuwa Klopp ataweza kuwa meneja mzuri mno baadaye.

Haas anasema walipokuwa wanasikiliza mpira kwenye Redio, mechi ya Bundasliga wakati huo, Klopp alianza kuchambua mbinu za Stuttgart na pia akatoa mawazo ya nini kifanyike katika sabu jinsi alivyoona yeye. Na punde wakasikia watangazaji wakisema mabadiliko yaliyofanyika ambayo ndiyo aliyopendekeza Jurgen. Alianzia mbali sio? Haas alimuona Jurgen tayarui alikuwa meneja wakati huo!
Klopp alikua katika mazingira ya kupenda soka na kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwa kiongozi. Alikuwa mchezaji mzuri na akapewa heshima na nafasi katika klabu ya Mainz kuwa kocha mkuu. Alifanmikiwa kuipeleka timu katika Bundesliga kwa mara ya kwanza. Mpaka sasa ana mafanikio makubwa katika soka na mataji mengi.
Soka lina watu wengi wenye historia ya kutoka kwenye mazingira duni na waliokuwa na ndoto kubwa ambao wengi wanaziishi ndoto zao. Jurgen Klop ni mfao wao.



Furahav
Na kweli huyu klopp anakipaji kikubwa sana.
Ester jackson
Aaah kweli kabisa kipaji cha mtu huazia akiwa mdogo