Barcelona na Messi Mchaka Mchaka Mkataba Mpya

Hii siyo mara ya kwanza kwa siku za hivi karibuni raisi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu kusisitiza Messi atasalia klabuni hapo.

Taarifa za Messi kutaka kuondoka klabuni Barcelona zinaendelea kuumiza vichwa vya mabosi wa Barcelona ambao wanajaribu kukanusha taarifa hizo kila wakati.

Inakumbukwa wiki kadhaa zilizopita Messi ametajwa kuwa kuna mambo fulani klabuni hapo yameshamtibua na anataka kuondoka. Awali messi alikuwa akijitokeza kukanusha taarifa zozote sisizo za kweli kuhusu hatma yake. Lakini kwa sasa amekuwa kimya zaidi kuzungumzia hilo baada ya kutajwa kuwa amechoshwa na baadhi ya mambo.

Messi kukaa kimya siyo kawaida, na hii inaongeza zaidi minongo’no juu ya hatma yake. Kimsingi kuna namna ambayo inaonekana klabu na Lionel Messi wanashindwa kufikia makubaliano.

Kwa mujibu wa raisi Josep Maria Bartomeu, klabu imeshajaribu kuongea na Messi na wanaendelea kuongea na nyota huyu kumshawishi juu ya kuongeza mkataba. Messi alikataa kusaini mkataba wa maisha klabuni hapo, na sasa kuongeza mkataba inakuwa ni kipengele kidogo.

Wadau wanadai kuwa kama Messi angekuwa na utayari na hana shida na kusalia Barcelona basi mazungumzo ya hatma yake yangekuwa yamekamilika, ukizingatia mda aliokuwepo klabuni hapo hii ni ishara kuna jambo huenda haliko sawa.

Barcelona wana imani wataweza kumshawishi kusaini mkataba mpya. Mkataba wake wa sasa unaisha mwaka 2021. Ametoa mchango mkubwa klabuni hapo tangia alipofika mwaka 2004.

“Tuliongea, tumeonga na tutaendelea kuongea na Messi. Atasaini tu mkataba mwingine naamini”

-Josep Maria Bartomeu

 


Kuna ofa kibao sana unzaofaidi ikiwa unabashiri na Meridianbet. Jiunge sasa kufurahia ofa zetu

Bonyeza HAPA Kujiunga

41 Komentara

    Asanten meridian kwa makara #Meridianbettz

    Jibu

    Huyu Messi Nae si Aje Man U#Meridinbettz

    Jibu

    Nadhani ni uvumi tu Messi hawezi kuondoka barcelona

    Jibu

    Messi awezi kuondoka Barcelona #meridianbet

    Jibu

    Ili Messi aondoe iyo minong’ono aseme ukweli

    Jibu

    Messi mfalme wa barcelona hawezi kutoka hapo

    Jibu

    Messi awez kuondoka Barcelona

    Jibu

    Watu wanapenda sana kuvumisha mambo ambayo siyakweli messi baki hapo hapo barcelona

    Jibu

    Barcelona fanyeni juu chini mbali na Messi

    Jibu

    Messi ni mfalume wa Barcelona hawezi kuama naimani hata staafu akiwa Barcelona

    Jibu

    Bora abaki bacrelona messi

    Jibu

    Messi nenda sehemu nyingine ukaonyeshe kipaji chako

    Jibu

    Barcelona wamekua na ufinyu wa mawazo sana hyu mess wanamuona km mungu wao kwa nn wasiangalie mbadala wake baadala ya kuendelea kung’ang’ania tuu mtu hataki yan imekua kama kuondoka kwa mess Barcelona imekufa hii ndio alikua haitak mzee sir Alex Ferguson mchezaji kua juu ya timu yeye ndio awe na saut anachotaka yeye ndio club mfanye wakati Barcelona ndio imemfanya akawa pale alipo sasa huu ni upuuz huu kama ningekua rais wa Barcelona uuza kabisa mess leta mtu atakae tengenezwa kua kama yeye baadae sio.muda wa kumbebeleza wee kama mnaomba uhai bwana yeye ndio alieshikilia maisha yenu

    Jibu

    Ni habari njema

    Jibu

    Bola messi abaki#meridianbettz

    Jibu

    Still atamalizia career yake hapo hapo.

    Jibu

    Ni mess mchaw tu kuhama Barcelona ni kitu kigumu sababu ni timu iliomtibu ugonjwa wake wa kudumaa hivyo ni kama analipa fsdhila

    Jibu

    Haindoke tu akapambane kwenye vilabu vingine.

    Jibu

    Kwel maana barca bila messi haiwezi fanya vizur

    Jibu

    Kweli Messi anategemewa aise

    Jibu

    Na lazima Asian na abaki barca tu

    Jibu

    Messi amenukuliwa mara kadhaa kuwa hahitaji kuondoka klabuni Barcelona. Ripoti zilitaja kuwepo kwa jitihada za kuhakisha Messi anasaini mkataba wa Kusalia Barca maisha yake yote ya soka. Lakini akanukuliwa akisema ‘hahitaji mkataba wa maisha’ klabuni hapo.
    Kama Messi akisaini mkataba wa maisha ina maana kuwa nyota huyu atasalia klabuni hapo hadi kustaafu soka lake. Lakini staaa huyu aliona bado siyo sahihi kwake kujifunga kiasi hicho na kuona huo sio mkataba mzuri kwake licha ya ukweli kuwa anaweza kuwepo hapo maisha yake yote hata bila mkataba wa namna hiyo.
    Messi aliweka wazi kuwa Barca walipendekeza asaini mkataba wa maisha, ila yeye aliona si sawa. Mwaka 2019 Akizungumza na Radio Metro Lionel Messi alisema
    Ni kweli Barcelona walinipendekezea mkataba wa maisha, lakini nilichokisema ni kuwa sitaki mkataba ambao unanifunga mimi kiasi hicho. Nahitaji kuwa sawa kuendelea kucheza, niendelee kupambania magoli hapa. Naweza kuwa hapa maisha yangu yote, lakini bila huo mkataba wa maisha. Naweza kuwepo hapa maisha yote.

    Jibu

    Bado anatafakari lakin kama Maelewano mazuri na viongozi wake anaweza kuondoka#meridianbett

    Jibu

    Habari njema! Kwa mashabiki Wake & team nzima#meridianbettz

    Jibu

    Habari nzuri.

    Jibu

    Messi tunakuomba usaini mkataba mpya na uendelee kubakia barcelona

    Jibu

    Hii ni habari mzuri

    Jibu

    Messi abak Tu

    Jibu

    Mess atamalizia soka lake barca

    Jibu

    Mess awez kuondok

    Jibu

    Maboss wanamkubal sana mess lazima waumize kichwa

    Jibu

    Messi Bora asepe tu ndani ya Barca

    Jibu

    Namkubali Sana Messi don’t leave barc.

    Jibu

    Afanye mpango wa kusepa kwenda kucheza sehemu nyingine

    Jibu

    Barcelona wanahaha sana mana messi akiondoka tu imekwisha

    Jibu

    Messi hawezi kuondoka Barca yy ndio kila kitu pale akiondoka sijui ht itakuwaje

    Jibu

    Messi hawezi kuondoka Barcelona ndiyo nyumbani na piya wanamtegemea Sana

    Jibu

    Sizani Kama Messi anaweza ondoka Barcelona

    Jibu

    Messi anajua wanamtegemea kwa kiasi kikubwa kunyamaza kwake ni km pozii tu ila kutoka Barcelona hatoki

    Jibu

    Mess kutoka Barcelona izo ni ndoto

    Jibu

    Kuondoka Barcelona Mess cyokweli

    Jibu

Acha ujumbe