Messi Hatarini Kupoteza Rekodi ya Supercopa

Nyota wa Barcelona Lionel Messi yupo kwenye hatari ya kupoteza rekodi yake ya Supercopa de Espana wikiendi hii kwa mujibu wa chapisho la Marca.

Nyota huyu ambaye anajitahidi kurejea katika hali yake shwari baada ya kupata jeraha wikiendi iliyopita, anaweza kuikosa mechi ya fainali ya Supercopa de Espana dhidi ya Athletic Bilbao Jumapili.

Kama Messi akiikosa fainali hii, itakuwa ni fainali ya kwanza ambayo BArcelona wanapambana bila kuwa na Lionel Messi tangia ile ya Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2006, ambayo Barca walipoteza dhidi ya Internacional wa Brazil.Mesi aliikosa mechi hii pia kwa sababu ya jeraha.
Lionel MessiTangia wakati huo, fainali zote 27 zilizofuata Leo alihusika dimbani. Fainali yeyote bila Messi kwa mashabiki wa Barcelona ni kitu ambacho hakifikiriki na kazi kujua nini kitafuata kutokana na umuhimu wake kwa takribani fainali zote alizocheza, lakini hili linaweza likatokea Jumapili hii.

Messi alipata jeraha la paja wiki iliyopita, na amekuwa akiendelea vizuri. Licha ya wasi wasi kuwa huenda kesho ikawa vigumu kwake kucheza. Anasafiri na kikosi cha Koeman, akipewa fursa ya kujaribu kujiweka sawa tayari kwa mchezo.


 

MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5

Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!

INGIA MCHEZONI

 

 

16 Komentara

    Washaanza kumfanyia vitimbwi sasa

    Jibu

    Jamani Messi

    Jibu

    Duuh sa itakuaje

    Jibu

    hana jipya

    Jibu

    Tusubiri tuone

    Jibu

    Inaonekana kama Barcelona haiwezi chochote bila Messi. Hili sio jambo la afya hata kidogo

    Jibu

    Pole sana messi

    Jibu

    Habari Mbaya kwa Messi na wapenzi wa Barca

    Jibu

    Daah sasa itakuwaje

    Jibu

    Mess noma

    Jibu

    Messi ameshuka kiwango tena

    Jibu

    sa itakuaje

    Jibu

    Messi noma

    Jibu

    Alikua na sifa kwa muda mwingi akiwa na Barcelona na lazima tujue kwamba kila lenye mwanzo lina mwisho

    Jibu

    Too bad for him

    Jibu

    Jamani atakuwa ameanza mwaka vibaya

    Jibu

Acha ujumbe