Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ndiye mchezaji pekee aliyekosekana katika mazoezi ya jana Jumatano katika uwanja wa Mo Simba Arena.
MeridianbetSport ilishuhudia wachezaji wa Simba wakishuka katika basi lao na kuanza mazoezi huku Kiungo huyo fundi akiwa hayupo katika jopo hilo.
Habari ambazo MeridianbetSport tumezipata kutoka kwa mmoja jopo ndani ya kikosi hicho nyota huyo hakuuungana na wenzake kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo ameyapata.
“Mkude ni kweli hayupo ana matatizo ya kifamilia na kocha amemruhusu kwenda nyumbani kuyatatua,”amesema mmoja wa jopo hilo ambaye hakutaka kuandikwa jina na kusema kuwa kocha wake Didier Gomes ndiye mwenye mamlaka ya kuzungumzia kutokuwepo kwake.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.