Morisson Ajiunga na FAR RABAT

Winga wa zamani wa vilabu vya Yanga na Simba kutoka nchini Tanzania Bernard Morisson amefanikiwa kujiunga na klabu ya FAR RABAT kutoka nchini Morocco kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Morisson amefanikiwa kujiunga na FAR RABAT baada ya kutemwa na klabu Yanga aliyofanikiwa kusaini nayo mkataba wa miaka miwili, Lakini klabu hiyo iliamua kuachana na raia huyo wa kimataifa wa Ghana.morissonWinga huyo wa kimataifa wa Ghana amejiunga na miamba hiyo ya soka nchini Morocco ambapo taarifa za awali zilikua zikieleza kua mchezaji huyo anaweza kujiunga na klabu ya Singida Foutanin Gate ya nchini Tanzania lakini dili halikufanikiwa.

Winga huyo amefanikiwa kujiunga na kocha wake aliyefanya naye kazi kunako klabu ya Yanga Nassridine El Nabi ambao walipata mafanikio makubwa kwa pamoja kama kubeba mataji matatu ndani ya msimu mmoja na kucheza fainali ya kombe la shirikisho Afrika.morissonTaarifa kutoka nchini Morocco zinaeleza kua mashabiki wa klabu ya FAR RABAT hawajapendezwa na dili la Morisson kujiunga na klabu hiyo, Lakini kocha Nabi ndio inaelezwa amependekeza usajili wa mchezaji huyo wa zamani wa Yanga.

 

Acha ujumbe