Morisson Atambulishwa Singida

Winga wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga raia wa kimataifa wa Ghana Bernard Morrison atatambulishwa ndani ya klabu ya Singida Fountan Gate leo.

Morisson ametambulishwa ndani ya Singida Fountain Gate zamani Singid Big Stars kama mchezaji huru baada ya kumalizana na klabu ya Yanga ambao amewatumikia kwa msimu mmoja akitokea klabu ya Simba.morissonWinga huyo wa kimataifa wa Ghana amekua Tanzania tangu mwaka 2019 hivo amekua na uzoefu wa kutosha katika ligi kuu ya Tanzania na hata michuano ya kimataifa hivo anaweza kuwasaidia Singida Fountain Gate.

Singida Fountain Gate kuelekea msimu ujao ambao watakua wakishiriki michuano ya kimataifa hivo wanasajili wachezaji wenye uzoefu na ubora ambao wataisaidia klabu hiyo na Morisson ni mmoja wao.morissonMchezaji huyo anatarajiwa kutambulishwa kesho pia mbele ya mashabiki wa klabu hiyo ambapo itakua ni Singida Big Day kama ambavyo wanaiita ikiwa ni mwaka wa pili klabu hiyo ikifanya tamasha hilo.

Acha ujumbe