Kane: Kijerumani Bado Kinanisumbua

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza ambaye kwasasa anakipiga klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani Harry Kane amekiri kua lugha ya nchini humo bado inamsumbua mpaka sasa.

Harry Kane ambaye anajiandaa kuiongoza timu ya taifa ya Uingereza katika michuano ya kombe la ulaya itakayopigwa nchini Ujerumani mwaka 2024 lakini lugha ya kijerumani bado inamsumbua kioindi hichi akiwa mgeni nchini humo.kaneMshambuliaji huyo alifanikiwa kujiunga na mabingwa wa soka nchini Ujerumani klabu ya Bayern Munich akitokea klabu ya Totenham Hotspurs kipindi cha majira ya joto yaliyopita.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza amesema kua hajafanikiwa kuanza masomo yake ya lugha ya kijerumani, Kwani mwalimu alikua ametoka kidogo lakini amesisitiza anapaswa kuanza masomo yake haraka iwezekanavyo licha ya kuelezwa kua lugha hiyo ni nguma ila atahakikisha anaendana na utamaduni haraka.kaneMshambuliaji Harry Kane ameonekana kuingia kwenye mfumo wa klabu ya Bayern Munich mpaka wakati huu, Kwani ameshafanikiwa kufunga mabao takribani manne mpaka sasa katika michezo ambayo ameitumikia klabu hiyo.

Acha ujumbe