Kiungo wa kimataifa wa Brazil anayekipiga kunako klabu ya Newcastle United Bruno Guimaraes inaelezwa yuko kwenye hatua za mwisho za kusaini kandarasi mpya ndani ya klabu hiyo.

Guimaraes ambaye alijiunga na klabu ya Newcastle mwaka 2022 mwezi Januari akitokeea klabu ya Olympique Lyon ya nchini Ufaransa na sasa yuko mbioni kumalizana na klabu hiyo inayofanya vizuri kwasasa.GuimaraesKlabu ya Newcastle inataka kumuongezea mkataba mpya mchezaji wake huyo ambaye ameonekana anafanya vizuri klabuni tangu ajiunge na timu hiyo mwaka jana mwezi na timu hiyo inataka kumpa mkataba mrefu ambao utamfunga klabuni hapo.

Taarifa zinaeleza kua klabu ya Liverpool walikua wanavizia saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil na walikaribia kunasa saini yake jambo ambalo limewafanya mabosi wa Newcastle kumuongeza mkataba kiungo huyo.GuimaraesKiungo Bruno Guimaraes amekua akihusishwa na vilabu mbalimbali tofauti na Liverpool ambapo hata klabu ya Real Madrid imehusishwa mara kadhaa na kiungo huyo hii ikiwa ni kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha katika klabu ya Newcastle United.

 



JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa