Bayern Munich imethibitisha kuongeza mkataba wa Thomas Muller hadi 2023. Mjerumani huyo mwenye medali ya Kombe la Dunia ni moja ya wachezaji waliokuwa kwenye mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba, na kwasasa ametia saini kwenye kandarasi mpya atakayohudumu kwa msimu mitatu akiwa Bayern Munich.
Pamoja na kuporomoka kwa uchumi kwenye michezo kwa sababu ya Corona, Bayern Munich imetoa taarifa kuhusu kumuongezea mkataba kipenzi cha mashabiki.
Muller amecheza jumla ya mechi 521, amefunga magoli 195 na assist 186 katika kipindi chake chote.

Taarifa hii imekuja siku kadhaa baada ya Hansi Flick kuwa Kocha mkuu wa klabu, hilo sio la kushangaza kwa inajulikana kuwa Flick ni mshabiki wa Muller dimbani na ndio maana amesaini kandarasi kwani Flick amesaini tayari kuwa kocha mkuu.


David pere
Ndio mida muagaka kwa kumaliza mpira wake
Asia Abdy
Muller kipenz cha watu
Neema juma
Waooo hiyo safii sana. Wamefanya vyema kumwongezea mkataba mpya
Rehema Dickson
Wamefanya vyema kumwongezea mkataba mpya
isha
Muller hongera sana
Issa
Muller apo ndio kwako munich safi sana