Nani ni Msenegal Bora Kutokea Premier League?

Je, ni Ba? Mane? Cisse? Kuna wachezaji wazuri sana kutokea Afrika Magharibi ambao wamepamba sana michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Hakika wana vipaji vikubwa sana na wameweza kufanya vyema wakiwa ndani ya Premier League.

Kwa leo tutaangazia wale waliotokea kwenye taifa la Senegal. Jumla ya wachezaji 37 wameshiriki mashindano hayo wakitokea Senegal. Mtu mmoja maarufu zaidi ni Aly Dia ambaye alikuwa wa kwanza kuiwakilisha nchi yake kupitia klabu ya soka ya Southampton mwezi Novemba mwaka 1996.

Cheikhou Kouyate, Sadio Mane, Ismaila Sarr na Oumar Niasse nao wamefanya hivyo hivyo msimu huu.

Mfungaji wa hatitriki ya mapema zaidi ndani ya Premier League, Mane alijitengenezea jina lake akiwa na Saints kabla hajahamia kwa Liverpool.

Yeye alikuwa ndiye mchezaji mmojawapo kati ya wachezaji watatu walionyakua tuzo ya Golden Boot katika msimu wa 2018/19 mara baada ya kupachika jumla ya magoli 22 na akasaidia upatikanaji wa mabao 29 huku akifunga mabao 80 kwa ujumla, hii ni zaidii ya mchezaji yeyote kutoka nchini kwao.

Kuna mabao bora sana yaliyofungwa ndani ya PL kwa kupitia mastaa kadhaa wa kutokea Afrika Magharibi akiwemo Sadio Mane, Papiss Cisse na Demba Ba

Demba Ba amefunga magoli 43 kwenye michuano hiyo na kushinda tuzo ya Premier League Player of the Month mwezi wa kumi na mbili mwaka 2011 akiwa na klabu ya soka ya Newcastle United, kabla hajahamia kwa Chelsea.

Papiss Demba Cisse aliwika sana akiwa pale St James’ Park, akapachika jumla ya mabao 13 katika mechi 14 alizocheza tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi Januari mwaka 2012 na akawasaidia The Magpies kumaliza msimu wakiwa nafasi ya tano.

Angalia takwimu za wachezaji wa Senegal

Mechi Magoli Assists
El Hadji Diouf 243 Sadio Mane 80 Sadio Mane 29
Mohamed Diame 239 Demba Ba 43 El Hadji Diouf 25
Cheikhou Kouyate 187 Papiss Demba Cisse 37 Cheikhou Kouyate 10
Sadio Mane 185 Henri Camara 31 Mame Biram Diouf 9
Abdoulaye Diagne-Faye 166 El Hadji Diouf 28 Henri Camara 8

 

Idrissa Gueye alikuwa ni mchezaji muhimu sana kwa Aston Villa pamoja na Everton, akiwa na umaridadi sana awapo uwanjani kwenye gemu zake alizocheza.

Mido mwenzake, Mohamed Diame alicheza mara 239 kwenye Premier League kwa klabu za soka za Wigan Athletic, West Ham United, Hull City na Newcastle, akiwa wa pili kutokea kwa El Hadji Diouf miongoni mwa wenzake wanaotoka taifa moja.

Ni nani aliwika sana ama anawika sana kwenye ligi akitokea huko Senegal?

  • Demba Ba
  • Papiss Demba Cisse
  • Mohamed Diame
  • Idrissa Gueye
  • Sadio Mane

23 Komentara

    Good news 👍

    Jibu

    Waoooo safi sanaa

    Jibu

    Safiiiii

    Jibu

    mane ni jembe la kila mtu

    Jibu

    mane is best soon atachukuwah mchezaj bora wa dunia

    Jibu

    Yuko pamoja

    Jibu

    Mane jembe namkubali sana

    Jibu

    Kwangu El hadji diof ndio mchezaj bora mpaka sasa

    Jibu

    Namkubali money

    Jibu

    👍👍

    Jibu

    Demba cisse is a phenomenal!!!

    Jibu

    🙌

    Jibu

    Sadio Mane

    Jibu

    Mane ni kiboka

    Jibu

    Vizuri 🤙

    Jibu

    Mane anatisha sana

    Jibu

    Mane ni jembe kali

    Jibu

    Sadio mane ndo namkubali

    Jibu

    Sadio mane the best player in senegal

    Jibu

    Mane noma.

    Jibu

    Safiii sana

    Jibu

    👍👍

    Jibu

    Habari njama hiii

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.