Wakati timu mbalimbali zikiendelea kupitia wakati mgumu kwenye Ligi, kutana na mwamba huyu hapa wa Italia kwasasa Napoli ambaye amebaki peke yake katika ligi hiyo ambaye hajapoteza mpaka sasa.

 

Napoli, Moto wa Kuotea Mbali.

Napoli ambayo ipo chini ya kocha mkuu Luciano Spalletti, jana walikuwa ugenini kukipiga dhidi ya AS Roma ya Jose Mourinho na kuifunga kwa bao 1-0 na kufanikisha kupata alama tatu muhimu ambazo zilikuwa muhimu kwao.

Spalleti na vijana wake wameendelea kusalia kileleni wakiwa na pointi 29 mbele kwa pointi 3 kwa bingwa mtetezi AC Milan ambaye yupo nafasi ya pili akiwa na pointi 26 baada ya kucheza michezo 11.

Bao hilo la kuihakikishia ushindi kwa Bapoli lilitupiwa kimyani na Victor Osimhen katika dakika ya 80 ya mchezo huku Roma wakishindwa kupiga hata shuti moja ambalo limelenga lango mpaka kumalizika kwa mchezo wakiwa nyumbani.

Napoli, Moto wa Kuotea Mbali.

Baada ya kupoteza mechi hapo jana, Roma amefikisha mechi 3 alizopoteza na yupo nafasi ya 5 kwenye msimamo na pointi 22.

Mechi inayofuata kwa Napoli wiki hii ni ya Ligi ya Mabingwa ambapo atakuwa nyumbani siku ya Jumatano kumualika Rangers huku akiwa amecheza mechi nne na kushinda zote na ndiye kinara wa kundi A.

Napoli, Moto wa Kuotea Mbali.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa