Nico Williams ameongeza mkataba wake na klabu hiyo kwa kipindi cha miaka kumi, hatua inayodhihirisha dhamira ya pande zote mbili kuendeleza mafanikio na kudumisha uaminifu kwa muda mrefu zaidi.
Nico Williams, mwenye umri wa miaka 22, ambaye ameibuka kuwa moja ya vipaji vya hali ya juu barani Ulaya, sasa ataendelea kubakia San Mamés hadi mwaka 2035. Hatua hii imekuja katika kipindi ambacho vilabu vikubwa kama FC Barcelona, Chelsea, na Liverpool vilikuwa vinamfuatilia kwa karibu, hasa baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika msimu wa La Liga 2024/25 na mashindano ya Euro 2024 akiwa na timu ya taifa ya Uhispania.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na klabu, Athletic Club imethibitisha kuwa mkataba huo mpya unajumuisha kipengele cha kutompoteza kirahisi mchezaji huyo, huku kifungu cha kuvunjwa kwa mkataba kikiwa kimepandishwa hadi zaidi ya €100 milioni.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Nico Williams alielezea furaha yake kwa kusaini mkataba huo mpya:
“Athletic Club ni nyumbani kwangu. Hapa ndipo nilikopokelewa na kulelewa kisoka. Nina furaha kubwa kuendelea kuwa sehemu ya familia hii kwa muda mrefu zaidi. Lengo langu ni kuisaidia timu kufikia mafanikio makubwa zaidi, ndani na nje ya Hispania.”
Kaka yake, Iñaki Williams, pia ni mchezaji muhimu wa Athletic Club, na uhusiano wao ndani na nje ya uwanja unaendelea kuwa chachu ya mafanikio ya klabu hiyo.
Nico Williams alijiunga na timu ya wakubwa mwaka 2021 akitokea akademi ya klabu hiyo na tangu wakati huo ameendelea kuwa mhimili muhimu, akifahamika kwa kasi yake, uwezo wa kupiga krosi, na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani.
Kwa sasa, mashabiki wa Athletic Club wana kila sababu ya kutabasamu, wakijua kuwa nyota wao mkubwa ameamua kubakia nyumbani kwa muongo mzima ujao.