Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael raia wa Ubelgiji amefunguka kuwa hakutakuwa na pengo lolote la kumkosa beki wake wa kati Lamine Moro kwenye mechi atakazokuwa nje kwa sababu ana zaidi ya wachezaji wawili wa kuziba nafasi hiyo.

Kocha huyo ameongeza kwamba tayari ameshawaandaa Kelvin Yondani, Andrew Vincent,’Dante’ na Ally Mtoni, ‘Sonso’ kwa ajili ya kuziba nafasi ya beki huyo Mghana.
Lamine amefungiwa kucheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara na kamati ya utendaji kutokana na kosa la kumrukia kwa makusudi na kumpiga teke kiungo wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto ambaye naye amefungiwa mechi tatu.
Eymael amesema kuwa hakutakuwa na pengo la Lamine hata kidogo kwa sababu wachezaji hao wawili ambao ni pamoja na Ally Mtoni ‘Sonso’ na Kelvini Yondani wanaweza kutumika katika nafasi hiyo na kucheza vizuri.
“Kwanza kuhusu Lamine ni mchezaji mzuri na ambaye nimemtumia sana kwenye mechi zetu lakini naona kukosekana kwake wala haitakuwa tatizo kubwa.
“Nasema hivyo kwa sababu Yondani amekuwa kwenye fomu ya hali ya juu, kwa hiyo anaweza kucheza na Makapu (Said) na wakawa na muunganiko mzuri tu kwenye mechi zote ambazo tutamkosa.
“Lakini pia namrudisha Sonso (Ally Mtoni) katika kundi na ana uwezo wa kucheza hapo, pia usisahau kuhusiana na Dante ambaye naweza kumtumia pia. Kwa hiyo utaona kwa kiwango gani hakutakuwa na madhara ya kumkosa,” alisema Eymael.


Shafii
Sikuzote kocha mzuri hua na mbadala wa mchezaji tokea mazoezini tunasubili matokeo mazuri tu kwa wanayanga
David Pere
Mabeki anoa wengi Ndio maana anatamba sawa tutaona Kama kweli wataziba pengo lake
Samiah
Wapo wengi mabeki ndio maana wanatamba
Fatuma kasomo
Tutaona kama wataziba pengo lake
Rehema
Sijui itakuwaje gonja tuone Kama wataziba Hilo pengo
mwakalosi
kocha wa utopolo bhn kijimwambafai
Evaluziga
Aya ngoja tuone hao wakuziba pengo
Elika
Yanga washafulia hawana jipya sasa
Hamidu
Yanga hakuna timu.! #meridianbettz
Antony Luseno
Atua nzuri kwa kocha huyu subiri tuone endapo kama watazaa matunda
Zeiyana
Hiyo ndio kazi yake kocha lazima hamtengeneze mchezaji mbadala..!mashabiki tunategemea matoke mazuri yanga afrika
Mariam mtandama
Asante meridianbet #kwa taarifa
Magdalena
Ata kama anao wa kuziba pengo lakini hawawezi kumfikia kiwango chake kimpira
Ester jackson
Imekaa powa sana katika vita lazima upambane na pia kama silaha zimeisha kuna njia mmbadala za vita pambana kocha tunataka kuona matokeo tofauti sio kufugwa ukocha unaujua panga majeshi
Genia Sikaluzwe
Yanga wamefuli sana sasahivi
Caroline
Yanga mbele zaidi…
Khadija
Yanga hamuna mambo tena mshafuria#meridianbettz
lombo
mmmh hatar
Dorophina
Ni kocha mzuri anajiandaa vizuri kwa kila tukio la upungufu wa wachezaji
felister
yanga mbele daima
Lydia Emmanuel Magoti
Yanga hamna kitu humo wajipange upya
Sadick
Dante anaweza kuziba gap vizuri. Yondani hawezi kuwa mbadala#meridianbettz
Devotha
Tunasubiri matokeo yako kocha naamini mambo yatakua mazurii
Ernest
Ngoja tuone pengo lale litaonekana au laah!!!!
isha
Tunasubili matokeo maneno mengi ya nini
Rehema
Goja tuone itakuwaje
Gabriel
Upande wng Sina shaka na huyu kocha luc Eymael
Rehema Dickson
Ndio maana anatamba sawa tutaona Kama kweli wataziba pengo lake
Hope mwaikuka
Yetu macho
Angelina
Yanga hamna jipya
Povel
Gud news
warda
Yaani Hii Timu bwana huwa hata siielewi#Meridianbettz
Frank Patrick
Daima mbele Nyuma mwiko…
Mwajuma
Ngoja tutaona maneno yake yanaukwelia au anazingua tu
Furahav
Wachezaji wa Yanga hawajitambui.
Amiri Kayera
Wanao mabeki wengne lkn pengo la lamine alinambadala makosa mengi
Ester jackson
Imekaa powa sana katika vita lazima upambane na pia kama silaha zimeisha kuna njia mmbadala za vita pambana kocha tunataka kuona matokeo tofauti sio kufugwa ukocha unaujua panga majeshi
Tahiya
Kocha siku zote pengo alizibiki labda mbadala ndio unafanyika
Njiku
Sawa baba acha tuone itakuwaje maana sisi mashabiki ndio tutaona kama pendo litazibiki au laa?
Salma
Upo vizuri kocha kwa kujiamin
Evaluziga
Ngoja tuone itakuaje
Sabrina
Maoni:Asante kwa taaria #meridianbettz
Fatina mfingi
Mmmh