“Nipo Fiti Sana!” - Kane

Mshambuliaji nyota wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane amesema kuwa kwa sasa anajisikia kuwa yuko vizuri kuliko kipindi chochote kile!

Kane jana amecheza mchezo wake wa 200 katika ligi kuu ya Uingereza huku akiisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham kwa goli lake la dakika ya 82 ya mchezo huo.

Mchezaji huyo ambaye ametoka kwenye majeraha ya muda mrefu, alionesha kiwango cha kuridhisha sana katika mechi hiyo kiasi cha kumvutia kila aliyepata nafasi ya kutazama mtanange huo.

“Nafikiri hiki ndicho mshambualiaji anapaswa kufanya, kufunga magoli na kuisaidia timu kuchukua alama tatu kwenye kila mchezo. Nafurahi kurudi katika orodha ya wafungaji leo”, alisema Kane katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Sky Sports muda mchache baada ya mchezo huo kumalizika.

Kane ambaye alikua nje ya uwanja kwa zaidi ya kipindi cha nusu mwaka kwa sababu ya majeraha, alionesha kiwango kikubwa mno katik mechi hiyo tofauti na wengi walivyotarajia kwamba ingemchukua muda kiasi kuyazoea mazingira ya uwanjani tena.

“Niko poa zaidi sasa kuliko kipindi chochote kile, nilipata nafasi ya kupona na kupumzika kutoka kwenye majeraha”, akaongezea  “Kufunga ni jambo linaloleta furaha sana duniani, imekua muda mrefu tangu nifanye hivyo kwa mara ya mwisho.”

Goli hilo la Kane katika dakika ya 82 ya mchezo, ni goli la 137 kwa Kane katika ligi kuu katika miaka 6 aliyocheza kama mchezaji wa kikosi cha kwanza.

Nyota huyo wa Tottenham ana malengo ya kufikisha jumla ya magoli 200 katika ligi ya EPL na hilo linaonekana li mbioni kuwezekana kama asipobughuziwa na majeraha ya mara kwa mara kwani mpaka sasa ana miaka 26 tu!

57 Komentara

    Jamaa anajiamini Sana Ndio maana Jana kawanyoosha vizuri kabisa

    Jibu

    Kane yupo vizuri naamini atafanya vzr zaid

    Jibu

    Yupo vizur

    Jibu

    Mungu azindi kumpa nguvu

    Jibu

    Safi sana Kane tunakupenda pia mashabiki

    Jibu

    vizuri Kane endelea kuwanyoosha

    Jibu

    Ni mojawapo ya wachezaji muhimu na tegemezi pale Tottenham

    Jibu

    Kane chapa kazi

    Jibu

    Huyu ndo mr spurs ataipa matokeo kuanzia sasa akirejea

    Jibu

    Ni mshambuliaji mzuri lakini kwa mfumo wa Mourinho kushambulia kwa kushitukiza anaweza asifikishe idadi hiyo ya magoli#meridianbettz

    Jibu

    Safi kune endelea kuwanyoosha

    Jibu

    Safii sana Kane mana nafikiri hiki ndicho mshambualiaji anapaswa kufanya, kufunga magoli na kuisaidia timu kuchukua alama tatu kwenye kila mchezo

    Jibu

    Hongera sana kane Mungu azidi kukupa nguvu

    Jibu

    Kwa mujibu wa sky news wametudhibitishia kuwa Harry kane yuko poa kabisa n habar nyema sana kwetu pia tunashukuru meridianbet Tanzania kwa taarifa ambaye njema sana kwan kutokana na hal yake tulijua hatoweza kucheza mechi ya dhid ya Tottenham na west ham siku ya Jana hivyo kama mashabiki wa Hotspur tunafurahia kumuona jembe letu raia wa England kurud akiwa na afya njema tena kutudhibitishia hali yake yuko fiti tena sana n habar njema kwenu
    maana tokea apatwe na majeraha takriban miez sita tuliamin atoweza kurud akiwa fiti kabisa ila no furaha kuona amerud akiwa yuko vzur zaid
    Have a great news 👍
    # meridianbet Tanzania

    Jibu

    Habari njema maana tokea apatwe na majeraha takribani miezi sita turijua kama hatoweza kurudi akiwa fiti kabisa

    Jibu

    Maoni:kane yuko vizuri na azidi kufanya vizuri

    Jibu

    mfumo wa Mourinho kushambulia kwa kushitukiza anaweza asifikishe idadi hiyo ya magoli#meridianbettz

    Jibu

    Harry Kane ni mchezaji mzur na jana amedhihirisha

    Jibu

    Ni habari njema kwa mashabiki Tottenham

    Jibu

    Talent player.meridianbettz

    Jibu

    Kane ni mahili Sana katika mpira lakini anabidi atulie kwanza ajisikilizie afya yake zaidi ndo arudi katika soka

    Jibu

    Kane safi sana nakukubali makali wangu

    Jibu

    Kane yupo POA sababu wanamatumain na profile ya Jose Mourinho ya kubeba mataji kila timu aliyopitah hivyo kane amamatumain kiu yake ya kubeba taj next season unawez ikatimiah kutokana na record ya Jose Mourinho ndo maana anajisikiah mtu mwenye fulan natumain lake kiu yake itakatwa msimu ujao kwa kubeba taji lolote baran ulaya thnks meridian bet kwa update za michezo

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri na anapokuwa langoni wma timu pinzani ni hatari mno

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Kwa mpira wajana kweli yupo vizuri

    Jibu

    Hajaongopa kweli kabisah kane ni mchezaji mzuri Sana pia mchezaji bora na mwenye nidhamu Asante kwa habar nzuri meridianbettz

    Jibu

    Safiii

    Jibu

    Ni Jambo zuri ni kheri urudi dimbani maana tulimic vitu vyako Kane

    Jibu

    Maoni:Harry Kane yuko vizuri jamaa anajua

    Jibu

    Mungu amjalie kane aendelee vizuri na azidi kufanya vizuri wakati wote.

    Jibu

    Good to hear this

    Jibu

    Hakuna mwanasoka asiyejua kazi ya mshambuliaji huyo wa uingereza ambaye anaekipiga tottenham habari zuri kwa wapenzi wa soka na kwa mashabiki wa tottenham

    Jibu

    Kane fundii

    Jibu

    Kene mshambuliaji mzuri Sana.💪

    Jibu

    Harry kane n mchezaj mzr wa kiingereza na timu ya taifa na club yake ya spurs

    Jibu

    Watu wengi wanatamani sana kumuona Kane akiwa fiti ndani ya dimba ili tuweze kupata burudani kamili

    Jibu

    Majeraha yalimzingua ila analijua Sana gori

    Jibu

    Kujiamini ndo mpango mzima#meridianbett

    Jibu

    Kane natumania ni kiungo Bora Sana, natumai na zaidi km anenavyo atafanya vzr Sana.

    Jibu

    Natumania Kane ni kiungo Bora Sana km anenavyo nafsin amerjea vema kwa sasa naamin ataendeleza ubora wake Zaid.

    Jibu

    huu msimu apumzike tu

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri sana

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Namkubali sana Kane#Meridianbettz

    Jibu

    Naona kane ameanza kufanya baraha

    Jibu

    Kane yupo vzr#meridianbettz

    Jibu

    Kane fundiii

    Jibu

    Kane uko vizuri
    Mashabiki tunamkubali sana

    Jibu

    Kane namkubali sana.

    Jibu

    Namkubali sana uyu jamaa

    Jibu

    Kane anajua

    Jibu

    Kane namkubal sana

    Jibu

    Jambo jema kane yuko vzur

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.