Alikuwa Akimkosha Zidane Kila Alipokuwa Dimbani kule Chelsea, Sasa wapo pamoja, pale pale Real Madrid!
Kabla nyota wa zamani wa Chelsea, Eden Hazard kutimkia Real Madrid, alishawahi kugonga vichwa vya habari kwa kusema kuwa Real Madrid ni klabu ya ndoto zake tangia alipokuwa mdogo.
Staa huyu alionesha matamanio yake ya kufundishwa na meneja Zidane ambaye pia kwa upande wake aliweka wazi kuwa nyota huyu alimkosha kila wakati alipokuwa dimbani.
Swali ni je, Zidane ameshindwa kumfanya Hazard aendane na Madrid au Hazard ndiye anaifelisha Madrid?
Wenyewe wanasema kuujua utamu wa asali ni lazima uilambe!
Zinedine Zidane, alibainisha kuwa alikuwa akimkubali nyota huyu kwa mda mrefu, alikuwa akimfikiria mara zote wakati yupo Chelsea na kuona kama ni mmoja wa wachezaji bomba zaidi. Hazard ameshindwa kwa kiasi fulani kufikia moja kwa moja matarajio ya Real Madrid. Unafikiri hii ni chungu-tamu? Yawezekana.

Hazard alikuwa akifanya makubwa pale Chelsea, akiwa ni mmoja wa wachezaji tegemezi zaidi wa kikosi cha Maurizio Sarri. Mashabiki wa Chelsea wanaelewa vyema hisia walizokuwa nazo pindi kikosi kinavyoingia dimbani kulisakata bila kuwa na Hazard.
Zidane anaamini Real wangeweza kumtumia vyema Hazard, lakini huenda wakahitaji mda zaidi kuona matunda ya moja ya sajili zao za gharama.
Kwa mujibu wa Zidane, Hazard bado kabisa hajafeli klabuni hapo. Anaamini ni changamoto tu ya majeraha aliyopitia imemkwamisha kuweza kumtumia vyema na bila shaka sasa atarejea kwenye umashuhuri wake wa kushambulia.
Real waliwekeza Euro milioni 100 kwa ajili ya kumpata staa huyu kutoka Chelsea msimu wa joto uliopita. Bila shaka kwa juhudi zake kwenye ligi ya Primia, Real walifikiri angalau wanaweza kupata mrithi wa pengo la CR7.
Staa huyu apewe mda. Lakini itendawili cha pengo la CR7 kinaendelea kuonekana ni kigumu kwa Zidane. Wacha apewe mda kidogo huenda akafanya maajabu zaidi La Liga.


felister
Hazard apewe muda nina Imani atafanya vizuri
Hamidu
Hazard bado mchezaji mzuri..tumpe muda atarudi kwenye ubora wake#meridianabettz
Mariam mtandama
Asante meridianbet #kwa taarifa
Zeiyana
Harzad n mchezaji mzuri ila tatizo ni mfumo ambao aliokutana nao ndo maana amejikuta anacheza chini ya kiwango ila kwa upande wangu wakimpa muda wa kuzoea mfumo kama alivyokuwa Chelsea harzad atatisha sana kwan wapenz wasoka kombe la dunia nameona alivyokuwa anakimbiza huku lukaku mbele harzan anatikisa nyavu hivyo naamin wakimpa nafasi ya kuzoea mfumo was Madrid atakuwa hatar
Magdalena
Madrid wanabidi wampe muda wa kutosha uku wakinsihii kurekebisha alipokosea
Leticia
Hazard ni mchezaji mzuri wampe muda
isha
Hazard yuko sahihi apate muda tuuu
Amani
anachotakiwa ni kujiamini zaidi atafanya makubwa ila hawezi kuwa mbadala wa CR7#meridianbettz
Povel
Hazard bdo sana ana huwez wa kucheza kandanda majerah ndo yamemwangusha na kufanya kuanza vbaya la liaga na mashindano mengne now mapemA sana kusemah kafel kikubw muda hatatuonyesha ubora thnks meridian bet btz kwa update
Issa
Hazard ni mzuri sema falsafa za zidane na mazingira ya madrid ajayazoea bado
Hivyo inabidi apate muda zaidi
Mariam mtandama
Asante meridianbet #kwa taarifa
Genia Sikaluzwe
Hazard yuko sahihi ila ni vema akapewa muda
Dorophina
Tnx meridian kwa taarifa za michezo
David Pere
Amefeli vibay mno maana Hana hata jipya la kutambia
Gabriel
Hazard ilifaa sana club yake ya zaman ya Chelsea kwan tokea aondoke
tunaona Kama achez kile kiwango ambacho alichokuwa akichezea
akiwa club ya Chelsea lakin kwa upande
wang nahisi mfumo wa Madrid unamfanya asiwe anaulewa but inapaswa apewe
muda zaid huenda akaja kuelewa na kucheza kwa kiwango kikubwa sana
Caroline
Hazard anaifelisha Madrid
Sadick
Bado ni mchezaji mzuri. anachotakiwa ni kujiamini zaidi atafanya makubwa ila hawezi kuwa mbadala wa CR7#meridianbettz
Angelina
Harzad yuko vizuri
Shafii
Hazard alileta mapepe uingereza alikua na wakati mzuri akiwa na club yake Chelsea ila Spain kumemkataa
farida ahmadi
Hazard ni mchezaji mzuri hivyo Real Madrid wasikate tamaa Bado waendelee kumpa mda Bado pia hana nafasi katika timu yake na hanaweza pia hat akaziba pengo la cr 7
Ester jackson
Hazard in mchezeja mzuri sana ila kutokana na majeraha yamemkwamisha ndiyo mana kiwango chake kinaonekana kimeshuka ila kama watampa nafasi tena na hazard akaitumia vizuri basi ninaamini hata mashabiki tutafurahia sana
Ester mmakasa
Hazard mbona bado Yuko fresh ila ni changamoto ndogondogo zinatokeaga mahali popote.
Hope mwaikuka
Wamvumilie tu kwanza
Njiku
Hazard ni mchezaji mzuri hahaha eti walitegemea atakuja ziba pengo la cr7 jamani hivi hazard azibe pengo la ronaldo?utani huu,zidane ni kocha mzuri sana ila hazard anatakiwa kuendana na real madrid maana anauwezo wakutosha
Neema hassan
Hazard mchezaji mahiri apewe muda wa kutosha..
Aziza mushi
Hazard ni mchezaji mzuri apewe muda atafanya vizuri tu.
Omary lukumbi
Mbeligiji huyu amefeli sana yan tofaut alivyo kua Chelsea na alipo kwepo sasa real Madrid amekua sio hazard yule wa Chelsea anae ondoka na beki watatu peke yake yupo kimya sana ameshindwa kuonyesha makali yake sijui hali ya hewa ajazoea au mfumo aendan nao
Ernest
Hazard bado anahitaji muda lakini sio kama amefeli ndani ya Madrid
Amiri Kayera
Ajawa na msim mzur apo ndo mpila ulivyo
Mwajuma
Tuvute subra labla atakaa poa
Johnmary joel
Wampe nafasi tena bado anaweza#meridianbett
Fatuma kasomo
Bado anahitaji muda sio km amefeli
mwakalosi
bado hajafeli ila anahitaji muda zaid wa kuaniniwa
Samira
Hazard bado ni mchezaji mzuri sana wampe muda na kumuamini atafanya vizuri zaidi
Agness
Aongeze bidii asifeli tena
Rehema
Asante meridianbet kwa taarifa
Elika
Apewe mda ajifikilie kwanza
christopher
Amefeli vibaya sana, na hili lilionekana mapema tu kabla hata ya kuhama kwake maana wachache sana kutoka uingereza wanaweza kufanya vizuri spain
warda
Hazard mwenyewe anahofu tu
Lydia Emmanuel Magoti
Hazard bado anaitaji mda sio Kama ameferi ndani ya madridi
Devotha
Hazard bado anauwezo sana apewe muda tu
Khadija
Hazard ni mchezaji mzuri tumpe muda atafanya tu vzr jamani tusifanye mambo kwa haraka#meridianbettz
Zeiyana
Harzad n mchezaji mzuri ila tatizo ni mfumo ambao aliokutana nao ndo maana amejikuta anacheza chini ya kiwango ila kwa upande wangu wakimpa muda wa kuzoea mfumo kama alivyokuwa Chelsea harzad atatisha sana kwan wapenz wasoka kombe la dunia nameona alivyokuwa anakimbiza huku lukaku mbele harzan anatikisa nyavu hivyo naamin wakimpa nafasi ya kuzoea mfumo was Madrid atakuwa hatar
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa #meridianbettz
Mwanahamisi
Asante meridian kwa taarifa
Samiah
Asifeli kwani aongeze bidiii
Furahav
Hazard apewe muda tu.
Theonestina
Hazard Yuko vizur tu
Amani
anachotakiwa ni kujiamini zaidi atafanya makubwa ila hawezi kuwa mbadala wa CR7#meridianbettz
Salma
Apewe muda atafanya vizur
Asia Abdy
Bado ana nafasi