Mchezaji wa Ajax Abdelhak Nouri ameweza kuongea baada ya kutoka koma, familia imesema.
Kaka yake amesema mchezaji huyo wa Uholanzi ameonyesha ishara kwa kutikisa kope japo bado hajaweza kuongea wala kutembea.
Nouri alipata matatizo katika ubongo katika mechi za kirafiki kabla ya msimu dhidi ya Werder Bremen Julai 2017.

Mchezaji huyo amewekwa koma baada ya tukio Julai 8 2017 lakini kwa sasa yupo nyumbani kwenye nyumba ya utengamao ambayo imejengwa kwaajili yake.
Kaka yake Abderrahim amekiri: “Mambo yanaenda vuzuri kwa Nouri, kwani kwasasa, anaamka, analala, anakula, anaketi lakini hwezi kutoka kitandani.
“Kwa wakati huu ana mfumo wake wa mawasiliano, ananyua kope zake japo hawezi kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Mabango yamekuwa yakionekana aktika dimba la Johan Cruyff na mamia ya mashabiki wa,efika nje ya nyumba baada ya kupata taarifa juu ya tukio.

“Anajua wapi alipo. Ni njema kwake kuwa kwenye mazingira anayoyajua akiwa na familia inamzunguka.
“Tunaongea na kuangalia mpira nae – anapenda hivyo. Kuna wakati anapata hisia kali lakini punde ana tabasamu, ni vizuri kwetu.”

