Paul Pogba Uelekeo Ni Upi?

Aliwahi kusema Mino Raiola, nikumuongelea Paul Pogba, kila mtu anacharuka. Safari hii, Pogba amezungumza mwenyewe, tunaelekea wapi sasa?

Ni uhalisia kuwa, Paul Pogba amebakiza miezi michache kukamilisha mkataba wa miaka 5 na Manchester United. Inasemekana United wameshamuwekea ofa ya mkataba mpya toka mwezi Julai lakini, Pogba na timu yake hawajatoa jibu lolote kwenye hilo.

Kuna sintofahamu hapa, Pogba lengo lake ni kuondoka bure mwishoni mwa msimu? Anawapa muda United kujiongeza kwenye ofa waliyoitoa awali? Au kunamchongo anausikilizia mahali? jibu halijulikani mpaka sasa.

Ishu mpya imejitokeza kwenye mazoezi ya kujiandaa na michezo ya timu za Taifa. Pogba amenukuliwa akisema kuwa, kiukweli, miaka mitano aliyokaa United haijamridhisha – hajaridhika kabisa.

Mwaka huu umeshaisha, hatutashinda chochote. Ninahitaji kushinda mataji, iwe na Manchester United au timu nyingine yeyote.

Kwa habari zilivyo, Paul Pogba anazivutia baadhi ya timu kubwa barani Ulaya vikiwemo pia vilabu vinavyocheza EPL.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe