Paris Saint-Germain (PSG) wanatarajiwa kuachana na Mauricio Pochettino wakati wa majira ya joto. Lakini haitakuwa rahisi, lazima watoboke kidogo.
PSG walitumia €22m kumfuta kazi Laurent Blanc mwaka wa 2016 na kumlipa Thomas Tuchel €8m walipomfukuza 2020.
Pochettino ndiye kocha anayelipwa zaidi Ligue 1; anapokea €1.1m kwa mwezi, akizidiwa na Diego Simeone, Pep Guardiola, Jurgen Klopp, Antonio Conte na Massimiliano Allegri pekee.
Kwa mujibu wa L’Equipe PSG italazimika kulipa €20m ikiwa wanataka kumuondoa Muargentina huyo na timu yake ya makocha katika majukumu yao.
Zinedine Zidane amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuchukua nafasi ya Pochettino iwapo atatimuliwa, huku Pochettino mwenyewe akihusishwa na Real Madrid kwa muda mrefu.
Kwa kuzingatia kuwa Carlo Ancelotti pia yuko Chini ya shinikizo kufuatia kichapo cha kufedhehesha 4-0 Clasico dhidi ya Barcelona wikendi iliyopita,mambo yanaweza kubadilika juu ya kibarua chake.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.