Nyota wa Paulo Dyabala anaweka wazi kuwa hakutaka kwenda klabu nyingine yeyote! Kwa sababu hiyo Dyabala aliamua kuzisubirisha klabu zingine bila kuwapa majibu kwa mda mrefu kwa kuwa alikuwa anasubiri wito kutoka klabu ya Juventus.
Mshambuliaji huyu aliungana jna Juventus akitokea Palermo mwaka 2015 kwa ada ya paundi milioni 40na mpaka sasa thamani yake imeongezaka zaidi ya mara mbili.
Nyota huyu alipatikana na maambukizi ya virusi vya Corona, na sasa ameripotiwa kuwa anaendelea vizuri. Amesema kuwa toka mwanzo alikuwa akifikiria kuwa kuna wito kutoka Juventus, na ndiyo wito ambao ataukubali wakati klabu zingine kadhaa zikiwasilisha nia zao za kumsajili.
Wakati akishauriana na watu wake wa karibu juu ya uamuzi anataka kuufanya wakati akiwa amepokea ofa kutoka Vilabu kadhaa, huku akipuuzia wito wa vilabu hivyo. Watu wake wa karibu walimuonya kuwa ingekuwaje kama angekosa kuitwa Juventus? Lakini yeye binafsi aliamua kutowajibu wala kufunga milango kwa klabu nyingine yeyote. Hadi alipopokea wito toka Juve.

“Siku moja nbaada ya chakula cha mchana, nilipokea simu kutoka kwa wakala wangu akaniambia ndani ya saa moja utapokea simu kutoka kwa mkurugenzi wa Juventus. Nikaongea na Fabio Paraciti na akaniambia atafanya kila awezavyo kufanikisha mimi kujiunga Juventus”
-Paulo Dyabala
Toka Paulo Dyabala ajiunge na Juventus nyota huyu mwenye umri wa miaka 26 amecheza mechi 216 za Juventus na kufunga magoli 91 na asisti 36. Ndoto yake ilikuwa kutua Juventus na alifanikiwa.


aisha
Duuuh jamaaa anaupendo na juventus