Paulo Dybala: Nasepa Msimu wa Joto

Mshambuliji wa Juventus Paulo Dybala amesema yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A msimu huu wa joto, kwa mujibu wa ripoti.

Mkataba wa Muargentina huyo unamalizika mwezi Juni, na kwa sababu hiyo, amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa vya juu vya Ulaya kabla ya uwezekano wa uhamisho wa bure katika majira ya joto.

Juventus wanatajwa kuwa wamekuwa na nia kubaki na staa huyu mwenye umri wa miaka 28 kwa muda, lakini hadi sasa wameshindwa kufikia makubaliano ya masharti mapya.

Paulo Dybala

Kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport, Dybala ana hakika kwamba Juventus hawahitaji tena huduma yake, na kwa sasa anasubiri ofa kutoka vilabu vingine.

Wakala wa Dybala aliripotiwa kukutana na Juventus kujadili mkataba mpya siku ya Alhamisi, lakini mkutano huo uliahirishwa hadi likizo ya kimataifa.

Miamba Inter Milan, Tottenham Hotspur, Barcelona na Manchester City wamehusishwa na kutaka kumnunua fowadi huyo.

 


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe