Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola ameongelea juu ya mustakabali wake huku akisema kuwa “Ikiwa nitabaki Man City ni sawa, Nisipobaki Man City klabu itakuwa kamili pia”, alikiambia Kituo cha michezo cha Sky Sports.
Kocha huyo ambaye amepata mafanikio mbalimbali akiwa na vilabu kadhaa amesema kuwa City ina nguvu na maamuzi wanayoyachukua ni mazuri pia.
Manchester City kadri siku zinavyozidi kwenda inazidi kuwa timu yenye ubora na imesajili wachezaji wenye ubora zaidi akiwemo Erling Haaland ambaye ametokea Borrusia Dortmund na ndiye kinara wa ufungaji mabao msimu huu.
Katika mechi saba ambazo wamekwishacheza,Pep na vijana wake wameshinda mechi tano, wametoa sare mbili na hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa. Mabingwa hao wa msimu uliopita kesho wataingia dimbani kuwakabili United katika Dabi yao ya jiji la Manchester.