Pep Guardiola anafurahi kuona Manchester City ikiwa na maendeleo mazuri chini ya uongozi wake tokea alipochukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo majira ya kiangazi mwaka 2016.
Mchezo wake dhidi ya Crystal Palace utakuwa mchezo wake wa 200 tokea atue kwenye viunga vya Citizens kama mkufunzi mkuu, katika michezo 199 aliyoiongoza City ameshinda 146, sare 25 na amepoteza michezo 28 tu, huku akiwa na magoli 486.

Katika misimu mitano aliyokuwepo City amechukua mataji matatu ya ligi kuu ya “EPL” huku akiweka kumbukumbu ya kipekee ya kufikisha pointi 100 kwenye msimu wa 2017-18, na kufanya kuwa msimu wakipekee kwenye klabu ya Man City.
“Nina furaha sana, kuona timu ikikuwa siku hadi siku hii ni ishara kuwa tunafanya vizuri najaribu kuzoea na kubadilisha baadhi vitu kwenye ligi kuu ya uingereza, baada ya mchezo wa 200 sitakuwa nimeridhika, imekuwa ajabu, tunaishi vile tunataka na tunafanya hivyo, nitajaribu kufanya hivyo” Pep Guardiola
Pep Guardiola ataingoza City jumamosi kwenye mchezo wake wa 200 kwenye ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Crystal Palace kwenye uwanja wake wa nyumbani Etihad, City anashika nafasi ya 3 akiwa na pointi 20 kwenye michezo 9 huku Crystal Palace akishika nafasi ya 15 akiwa na ponti 9 kwenye michezo 9 ya “EPL”.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.
CHEZA HAPA