Inter Milan wametangza kumuweka kiungo wao mshambuliaji Christian Eriksen sokoni kutokana na sheria za Serie A zinazomzuia kutokucheza mashindano yeyote kwenye ardhi ya Italia.
Christian Eriksen ambaye alianguka kwenye mchezo wa EURO 2020 dhidi ya Finland na kuwaishwa hospitali kutokana na tatizo la kusima kwa mapigo ya moyo, na kupatiwa matibabu na kuweka kifaa maalumu ambacho kinasimamia mwenendo wa mapigo ya moyo ICD (implantable cardioverter defibrillator).
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Inter Milan, “tukirejea haki ya usajiri wa Eriksen, kutokana na titizo lake lilitokea kwenye mashindano ya ulaya juni 2021, anazuiliwa na mamlaka ya utabibu kujihusisha na michezo yote kwa sasa nchini italia.”
“Ingawa kwa hali aliyokuwa nayo anaweza kuruhusiwa kucheza sehemu nyingine na anweza kufanikwa katika nchi nyingine na kuendelea na kazi yake kama kama kawaida.”
Eriksen ameichezea Inter Milan michezo 60 na kuifungia magoli 8 na pia amekuwa mmoja wa wachezaji walioisaidia Inter kuweza kuchukua ubingwa wa Serie A
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.
CHEZA HAPA