Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amelezea kusikitishwa na na hali anayopitia kocha mwenzake Thomas Tuchel baada ya mmiliki wa klabu hiyo kuwekewa vikwazo na serikali ya Uingereza ambavyo vimeasili klabu hiyo.
Tukio la kumewekewa vikwazo Roman Abramovich ni kujibu mapigo ya serikali ya Urusi kuivamia nchi ya Ukraine, na wamezuia mali zote za mmiliki huyo ambazo ziko nchini Uingereza ikiwemo klabu ya Chelsea.

Klabu ya Chelsea itafanya kazi kwa kibali maalum, kwenye vikwazo ambavyo vilivyowekwa kwenye klabu hiyo ni pamoja na kutouza tiketi, wakati serikali ikiweka wazi swala la kuuza klabu hiyo ambapo kwenye mauzo hayo Abramovich hatarajiwi kupata chochote.
Guardiola anahisi ni swala gumu sana kwa kocha wa klabu ya Chelsea kuweza kupambana nalo, “ni nafasi ngumu kwa kocha Thomas Tuchel na wachezaji,” alisema kwenye kikao na waandishi wa habari.
Aliongezea Pep Guardiola “Huwezi kuwa sawa na najisikia vibaya kwao sababu inabidi wako pale kufanya kazi kwa kadri iwezekanavyo, kilpokuwa na korona tuliombwa kuongea kama madaktari kwenye dawa, chanjo tulikuwa tunaizungumzia kama tunajua kila kitu.
“Sisi ndio sura ya klabu, tupo hapa kila baada ya siku tatu, kwaiyo unauliza chochote unaachotaka, mnapaswa kujua kuwa kuna vitu hatuvifahamu, na hatuna muda wa kuvisoma na kuvizungumzia kwa vile mnavyouliza.” Aliongezea Pep Guardiola
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


