Mauricio Pochettino kwa mara ya kwanza amebeba kombe kwenye maisha yake ya kuwa kocha. Muagentina huyo ameondoa ukata baada ya PSG kuwaburuza Marseille jana usiku.
PSG walikuwa wakichuana na Olympic Marseille kwenye fainali ya kombe la Trophee des Champions ukiwa ni mchezo wa 3 kwa Pochettino tangu akabidhiwe kikosi cha timu hiyo.
Trophee des Champions ni kama kombe la Ngao ya Hisani kule EPL ukimkutanisha bingwa wa ligi dhidi ya bingwa wa kombe la ligi kwa msimu uliopita.

Magoli ya Mauro Icardi na Neymar Jr yaliwatosha PSG kuwazidi kete Marseille licha ya Dimitri Payet kupachika goli 1 la kufutia machozi.
Ushindi kwa PSG umeendeleza umwamba wa timu hiyo kwenye soka la Ufaransa, hili linakua kombe la 19 kati ya 20 ambayo PSG wamecheza hatua ya fainali kwenye mashindano ya ndani. Hii ni mara ya 8 mfululizo kwa PSG kubeba taji la Trophee des Champions.
MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5
Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!



Shakila mrope
Habari njema
Sania
Hongera Pochettino
Sadick
Hongera PS. Ni mwanzo mzuri kwa Pochettino, wahenga wanasema nyota njema huonekana asubuhi
Caroline
Hongera sana Pochettino
Rahmal
Pongezi kwako pochettino
Magdalena
Safi Sana kwa kazi nzuri
Dorophina
Pongezi kwao PSG
Saupha mohamed
Hongera
Mwanahamisi
Hongera zao
Issa
Huyu ndie kocha
Angelina
Safi
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
felister
pongezi kwk
Hopemwaikuka
Hongera zenu
Sarah
Pongezi kwao
warda
Hongera yake