Pogba Amekata Tamaa Kusepa Man United?

Paul Pogba aliweka wazi kuwa anahitaji kusepa Man United na kusema kuwa angependa kupata changamoto mpya mahali tofauti na Old Trafford.

Hata hivyo kufungwa kwa dirisha la uhamisho kwa klabu za EPL kumemkuta staa huyu akisalia Man United. Klabu alizohusishwa nazo ilikuwa ni Real Madrid baada ya Zidane kusema Pogba ni moja ya wachezaji anaowahitaji. Juventus pia walitajwa kuwa kwenye mchakato wa kutaka kumrejesha staa huyu.

Wakati Hatma yake kusalia United ikiwa na viulizo vingi, Pogba ameshiriki vyema kuisaidia klabu yake kwenye mechi ya kwanza ya EPL msimu huu na kuchangia pasi 2 za magoli walipowachakaza Chelsea bao 4-0.

Akizungumzia hatma yake, Pogba anasema kuwa mpaka sasa kuna maswali mengi ambayo bado hayana majibu, ila kiuhalisia yeye yupo klabu ya Manchester United.

Ameongezea kuwa yeye wakati wote anafurahia kucheza soka, na anapenda anachokifanya, pia ana furaha kuwa na wachezaji wenzake wa Manchester United.

Bila shaka, baada ya kushindwa kupata uhamisho wa mapema, Pogba hana matarajio makubwa sana ya kusepa klabuni hapo kipindi hiki na amepanga kufanya jitihada zake klabuni United. Kama kutakuwa na mabadiliko itakuwa heri kwake pia.

Makala iliyopita

4 Komentara

    Pobga abaki tu Manchester United kwani bdo anahitajika #Meridianbettz

    Jibu

    Abaki man u bado mchango wake unaitajika

    Jibu

    Aende tu.

    Jibu

    Baki tu hapo.

    Jibu

Acha ujumbe