Potter Kuibukia Leicester City

Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Uingereza Graham Potter anahusishwa kwa karibu kujiunga na klabu ya Leicester City kuelekea msimu ujao wa 2024/25.

Klabu ya Leicester City ipo kwenye mazungumzo na Graham Potter na hii ni baada ya kupita wiki kadhaa kuondokewa na kocha wao aliyewapandisha daraja Enzo Maresca ambaye amejiunga na klabu ya Chelsea kwa mkataba wa muda mrefu.potterKocha huyo wa kimataifa wa Uingereza amekaa msimu mzima bila kua na timu ambapo klabu ya Leicester City inaonekana inapmbana kumrejesha kazini kocha huyo wa zamani wa Brighton and Hove Albion, Kocha huyo ni kweli hakua na wakati mzuri ndani ya klabu ya Chelsea lakini wengi wanatambua uwezo wake akiwa ndani ya klabu ya Brighton.potterMpaka sasa mazungumzo yanaendelea baina ya kocha Graham Potter na klabu ya Leicester City wakati huohuo klabu hiyo pia inafanya mazungumzo na makocha wengine, Lakini Leicester City wanampa nafasi kubwa kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Chelsea na Brighton Hove and Albion.

Acha ujumbe