Musiala: Nataka Tuwe Washindani

Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayekipiga ndani ya klabu ya Bayern Munich Jamal Musiala ameulizwa juu ya mkataba mpya ndani ya klabu hiyo, Lakini yeye amesema malengo yake ni kuona timu hiyo inacheza mpira mzuri wa kuvutia na kua washidani kwenye ligi ya mabingwa ulaya.

Jamal Musiala anaeleza kama timu itakua kwenye ubora na kucheza mpira wa kuvutia na kua shindani haswa kwenye michuano ya ulaya, Basi hivo ndivyo ataweza kuonesha ubora wake ndani ya miamba hiyo ya soka kutoka nchini Ujerumani.

 

Kiungo huyo kwasasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ujerumani akijiandaa na michuano ya Euro inayotarajiwa kuanza mwezi huu tarehe 14, Kutokana na ambayo ameyaongea Jamal Musiala ni wazi kwasasa hafikirii suala la mkataba mpya zaidi akili yake inaweza ni namna gani timu hiyo itarejesha makali yake na kua timu shindani haswa kwenye michuano ya ulaya.musialaKiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Fc Bayern Munich kwa misimu miwili sasa, Kiungo huyo anamaliza mkataba wake mwaka 2026 ina maana kabakiza misimu miwili tu ndani ya mkataba wake na kwa namna anaonesha ubora ndani ya timu hiyo ni wazi klabu hiyo itaanza mazungumzo ya mkataba mpya hivi karibuni.musialaKiungo Jamal Musiala pia anahusishwa na klabu ya Real Madrid pamoja na Barcelona na mkataba wake unamalizika mwaka 2026, Hivo klabu ya Bayern Munich inapaswa kua makini kwani vilabu hivo vinaweza kumsajili mchezaji huyo ambaye amekua kwenye kiwango bora sana klabuni hapo na kua moja ya wachezaji bora ulaya.

Acha ujumbe