PSG: Messi KUBAKI, Poch KUONDOLEWA!

Licha ya kutwaa ubingwa wa Ligue 1 kwa mara ya 9, PSG bado hali mbaya kati ya klabu na mashabiki wao. Mahusiano sio mazuri kati ya pande hizi.

Jumamosi wiki iliyopita PSG walijihakikishia ubingwa wa Ligue 1. Kutwaa ubingwa bado haikua sababu ya mashabiki kuungana nao, walionesha hisia zao kwa kuondoka uwanjani dakika 10 kabla ya mchezo huo kumalizika na, walienda kushangilia ubingwa nje ya uwanja.

Huu ni muendelezo wa mashabiki wa klabu hiyo kuonesha hisia zao kwa klabu hiyo ambayo, licha ya kufanya usajili mkubwa, hawana mafanikio wala kuonesha dira ya kufanikiwa kwenye Ligi ya Mabingwa.

Mashabiki wa PSG baada ya timu yao kutwaa ubingwa wa Ligue 1.

Hisia za mashabiki zinaungana na kile wanachokipitia viongozi wakubwa wa klabu hiyo ambao wanaripotiwa kuwa kwenye mpango wa kupangua kikosi kwa sehemu kubwa mwishoni mwa msimu huu.

Kylian Mbappe anahusishwa na Real Madrid huku Neymar Jr akifunguliwa milango kuondoka klabuni hapo kama kuna timu inamuhitaji. Ni Lionel Messi pekee anayepewa nafasi ya kubaki klabuni hapo wakati huu ambao, Mauricio Pochettino na Leonardo wakiwa kwenye hatihati ya kuondolewa klabuni hapo.

Huenda kukawa na kocha mpya ambaye atakabidhiwa timu kuanzia msimu ujao na, PSG itajengwa upya kumzunguka Lionel Messi.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe