Pengine hajaonekana akiwa kwenye uzi wa Manchester United lakini, Erik Ten Hag yupo kazini kimya kimya. Kazi inaendelea chini ya kapeti.

Ni wiki 1 toka Manchester United ilipomtangaza Erik Ten Hag kama kocha mpya wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao. Japokuwa bado anaendelea na kibarua chake kule Ajax, nyuma ya pazia, kocha huyu anapanga michakato yake kule Old Trafford.

Inasemekana, wachezaji wa United wamegawanyika baada ya taarifa rasmi za kocha mpya. Wapo wanaofurahia ujio wa Erik na, wapo ambao hawajapendezwa na hilo. Kwa lugha ya kimtaa, United kuna ‘Team Pochettino’ na ‘Team Erik’. 

Poch (kushoto) na Ten Hag (kulia).

United na Ajax wote wamebakiza michezo 4 tu kumaliza msimu huu kwenye ligi zao. Kwenye orodha ya majukumu ya Ten Hag, kituo kinachofata ni Zoom. Kocha huyu anampango wa kufanya kikao kwa njia ya mtandao (Zoom Meeting) na wachezaji wote wa Manchester United, kila mmoja kwa wakati wake lengo likiwa ni kutaka kuwafahamu zaidi wachezaji na utayari wao klabuni hapo.

Wapekuzi wanaendambali kwa kudhani kuwa, huenda hii ni mbinu ya kutaka kujua nani atamfaa na nani hamfai kuanzia msimu ujao (kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa), pamoja na hilo, kuna suala la nahodha wa timu – huenda Harry Maguire akavuliwa unahodha na kupewa mchezaji mwingine ambaye Erik atamuona anamfaa kwenye timu yake.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa