Chiellini Athibitisha Kustaafu Kuchezea Timu ya Taifa

Nahodha wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini amethibitisha kwamba atastaafu kuichezea timu ya taifa ya  Italia mwishoni mwa msimu huu baada ya kumenyana na Argentina katika uwanja wa Wembley Juni 1.

Beki huyo wa miaka 37 amecheza mechi 116 na timu ya taifa huku akiwa ameweka kambani bao 8 akiiwakilisha Italia kwenye michuano sita akifika fainali mbili na akifanikiwa kutwaa taji la Euro 2020 kwa kuifunga Uingereza katika uwanja wa Wembley mwaka jana.

“Nitacheza na kuiaga timu ya taifa huko Wembley, mahali ambapo nimekuwa na nyakati nzuri na huenda katika muda wote wa kazi yangu ushindi ule ulikuwa maalum.” Chiellini aliiambia DAZN baada ya kushinda dhidi ya Sassuolo siku ya Jumatatu.

“Ninahakika huu utakuwa mchezo wangu wa mwisho kwa timu ya taifa, ni wakati wa kuachia nafasi kwa wachezaji wengine wazuri.

Italia wameshindwa kufuzu kucheza kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo ambapo michuano hiyo mikubwa inatarajiwa kuanza kurindima mwezi Novemba mpaka Disemba mwaka huu huko Qatar.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe