PSG Wakomalia Windo la Ousmane Dembélé

Paris Saint Germain – PSG wanaripotiwa kuwa wanakomaa kuhakikisha wanafanikisha kumchukua Ousmane Dembélé kutoka Barcelona.

Kwa jinsi mambo yalivyo Barcelona, mpaka sasa Ousmane Dembélé haelewi hatma yake klabuni hapo.

Barcelona wanataka kusalia na staa huyu kwa kurekebisha vipengele vya mkataba, huku staa huyu akionekana yupo mbioni kusaini mkataba mpya na mabosi wake wa sasa.

Hata hivyo, staa huyu kwa sasa anaweza kufanya mazungumzo na kusaini makubaliano ya awali na klabu yeyote kuelekea masika. Kwa maana hii Barcelona wapo kwenye hatari ya kumpoteza ikiwa kuna klabu itakuwa na ofa bora zaidi.

kwa mujibu wa chapisho la Mundo Deportivo, PSG wapo macho kufuatilia ikiwa dili la kuongeza mkataba mpya na Barcelona litafaulu au litabuma. Ikiwa dili hili litabuma, basi wao wataingia miguu miwili.

Ripoti zinataja kuwa PSG wanafanya mawasiliano ya mara kwa mara na wakala wa Dembele.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe