Rafael Leao Awaingiza Vitani United na Chelsea

Mshambuliaji wa klabu ya Ac Milan na timu ya taifa ya Ureno Rafael Leao ameviingiza vitani vilabu vikubwa vya Manchester United na wababe wa London Klabu ya Chelsea.

Mchezaji huyo atari ambaye amekua miongoni mwa wachezaji tegemezi kwenye klabu ya Ac Milan chini ya mwalimu Stefano Pioli amekua kwenye ubora mkubwa mpaka kufanya vilabu vikubwa ulaya kugongana vikumbo ili kupata saini yake.rafael leaoIliripotiwa hapo mwanzo kua klabu ya Chelsea inahitaji huduma ya winga huyo matata wa kimataifa wa Ureno lakini taarifa za hivi punde ni kua mashetani wekundu nao wanameripotiwa kumfukuzia Rafael Leao na yupo kwenye mipango yao.

Klabu ya Ac Milan ina wakati mgumu sana kuweza kumbakiza mchezaji huyo bora wa Serie A msimu uliomalizika kutokana na ubora ambao amekua kionesha klabuni hapo, Huku vilabu vikubwa vikiwa vinamtolea macho na kuhitaji saini yake kwa udi na uvumba.rafael leaoWinga Rafael Leao ambaye alikua mchezaji mwenye mchango mkubwa sana wakati Ac Milan inabeba ubingwa wake wa kwanza wa Serie A baada ya miaka 11, Inaelezwa klabu ya Ac Milan inapanga kumpa mkataba mpya aweze kusalia klabuni hapo.

Acha ujumbe