Ronaldo Arejea Madrid Baada ya miaka minne

Nyota Cristiano Ronaldo kwa mara ya kwanza amerejea ndani ya Real Madrid leo siku ya jumatano tangu alipoondoka klabuni hapo kwa mara mwaka 2018.

Nyota huyo ambaye kwasasa hana timu baada ya kuachana na klabu yake ya Manchester United ameonekana kwenye viwanja vya kufanyia mazoezi vya klabu hiyo vinavyojulikana kama Valdebebas akifanya mazoezi leo.ronaldoNyota Cristiano Ronaldo ni mchezaji mwenye heshima kubwa ndani ya klabu ya Real Madrid akiondoka klabuni hapo akiwa kama mfungaji bora wa muda wote akiwa na mabao 450, Huku akiiwezesha klabu hiyo kubeba mataji mbalimbali ikiwemo mataji manne ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Kutokana na heshima ambayo anayo gwiji huyo ndani ya klabu hiyo imekua jambo jepsi kwa yeye kuruhisiwa kufanya mazoezi ndani ya viunga vya Valdebebas wakati huu ambao anasubiri kuangalia hatma yake siku za mbeleni.ronaldoInaelezwa Ronaldo amekua na mahusiano mazuri na rais wa klabu hiyo Florentino Perez na ndio alieruhusu mchezaji huyo kufanya mazoezi katika viwanja hivo wakati huu anasubiri kuangalia atatimkia timu gani baada ya kuachana na Man United.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.