Baada ya timu ya taifa ya Ureno kutupwa kwenye michuano ya kombe la dunia siku ya jana dhidi ya timu ya taifa ya Morocco nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo amezungumza jambo.

Timu ya taifa ya Ureno jana ilikutana na kipigo cha kushangaza kutoka kwa Simba wa milima ya Atlas kama wanavyojiita timu ya taifa ya Morocco, Na kupelekea timu hiyo kutupwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika mchezo huo wa robo fainali.ronaldoWachezaji wengi wa timu ya taifa ya Ureno wameonesha kusikitishwa kwa kiwango kiubwa baada ya kutupwa nje ya michuano hiyo, Lakini mtu aliekua anasubiriwa atoe neno baada ya kipigo hicho ni nahodha wa timu hiyo Cristiano Ronaldo ambaye kupitia mtandao wake Instgramu ameandika ujumbe mzito.

Staa huyo ameeleza kua ndoto yake kubwa kwenye naisha yake ya mpira wa miguu ilikua ni kuchukua taji la kombe la dunia na timu ya taifa ya Ureno, Lakini ameonesha kusikitishwa kwani ndoto hiyo haikuweza kufanikiwa na jana rasmi ndoto hiyo ilikufa baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo.

Staa huyo anaeleza amekua akipambana kila siku kwa zaidi ya miaka 16 akishiriki michuano hiyo mara 5 ili kuhakikisha anapelekea taji hilo kwa taifa lake analolipenda lakini haikua hivo kama ambavyo alitarajia kitu ambacho kimemuumiza kwa kiwango kikubwa sana.ronaldoRonaldo hajaweka wazi kua kama ataachana na timu ya taifa ya Ureno lakini amewashukuru raia wote wa Ureno ambao wamekua wakimpa ushirikiano kipindi chote alichokua anaitumikia timu hiyo, Wachezaji wenzake ambao alipambana nao kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha anakamilisha ndoto hiyo.


Staa huyo pia ameeleza anajua mambo mengi yatasemwa na kuandikwa lakini lengo lake kwa taifa hilo haliwezi kubadilishwa kwajili ya hichi ambacho kimetokea jana, Kwani yeye ataendelea kutoa ushirikiano kwa timu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa