Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Edison Arantes Do Nascimento Pele amemtaka mchezaji wa sasa wa timu hiyo Antony anayekipiga katika klabu ya Manchester United kutokata tamaa.
Staa huyo anayekipiga katika klabu ya Manchester United alishusha ujumbe wake mrefu katika mtandao wake wa Instagram na kueleza namna amehuzunishwa na timu yake kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia siku ya ijumaa.Timu ya taifa ya Brazil ilitupwa nje ya michuano ya kombe la dunia na timu ya taifa ya Croatia kwa mikwaju ya penati kitu kilichoishtua dunia kwani Brazil ilikua nim miongoni mwa timu ambazo zilipewa nafasi kubwa kutwaa michuano hiyo, Lakini waliishia kutolewa katika hatua ya robo fainali.
Baada ya Antony kuandika ujumbe huo gwiji Pele aliienda kwenye sehemu ya kutoa maoni na kuandika “Wewe ni sehemu ya kizazi kinachokuja. Usikate tamaa, Kua na nguvu, Na historia ndio imeanza” Gwiji huyo aliandika ujumbe huo kumtaka Antony kutokata tamaa kwani safari ndo kwanza imeanza kwa upande wake.Gwiji Pele ambaye kwasasa inaelezwa amewekwa sehemu maalumu kwajili ya kumpunguzia maumivu juu ya ugonjwa wake unaomkabili, Ambapo inaelezwa hauna tiba tena na kinachofanyika kwasasa ni kumpunguzia maumivu.