Pele Atuma Ujumbe kwa Neymar

Gwiji wa soka ulimwenguni na staa wa timu ya taifa ya Brazil Edison Arantes Do Nascimento maarufu kama Pele ametuma ujumbe kwa staa wasasa wa timu ya taifa ya Argentina Neymar Jr baada ya kufikia rekodi yake ya ufungaji mabao kwenye timu ya taifa ya Brazil.

Mshambuliaji Neymar jana alifanikiwa kufikia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwenye timu ya taifa ya Brazil ya gwiji huyo bvaada ya kufunga bao jana katika mchezo wa robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Croatia.peleNeymar alikua amebakiza bao moja kufikia rekodi ya gwiji huyo ambaye alikua ana jumla ya mabao 77 kwenye timu ya taifa ya Brazil, Hivo Neymar ambaye alikua ana mabao 76 kabla ya kufunga katika mchezo wa jana na kufikia rekodi ya gwiji huyo ambaye rekodi hiyo ilidumu kwa takribani miaka 50 mpaka kuja kuvunjwa na Neymar.

 

Kufuatia Neymar kuvunja rekodi ya gwiji huyo Pele aliandika kupitia mtandao wake wa Instagram kwa kumpongeza Neymar kuweza kuvunja rekodi hiyo, Lakini akieleza wazi haikua siku nzuri kwa mchezaji huyo na taifa la Brazil kwani walitolewa kwenye mchezo wa Robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Croatia.pelePele amemtaka Neymar aendelee kupambana kwakua alichokifanya kitavutia na kuwapa nguvu vizazi vijavyo kama ambavyo yeye alifanya miaka 50 iliyopita na mpaka leo rekodi zake zinaishi. Gwiji huyo amemtaka Neymar aendelee kufanya anachofanya kwani kinavutia mamilioni ya watu na kupitia yeye anawapa nguvu na kuamini vitu vilivyoonekana haviwezekani vinawezekana.

Acha ujumbe