Kaka: Awashangaa wanaomsema Ronaldo

Kiungo wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Ricardo Kaka ameshangazwa na namna watu wanavyomsema vibaya staa mwenzake wa zamani wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Gwiji Ricardo Kaka anaeleza kusikitishwa na vitu ambavyo vinaendelea kwasasa kumhusu Cristiano Ronaldo, Hii imekuja baada ya siku za hivi karibuni staa huyo kuonekana anapitia kipindi kigumu kwenye maisha yake ya mpira na kufanya vyombo vya habari mbalimbali kuandika vibaya kuhusu staa huyo.kakaRonaldo ndani ya mwaka 2022 amepitia wakati mgumu kwenye maisha yake ya mpira akishuhudia akishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha United, Kufiwa na mwanaye, Pamoja kushindwa kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kubeba kombe la dunia baada ya kutolewa mapema kwenye hatua ya robo fainali.

Gwiji Kaka anasema Ronaldo anapitia kipindi kigumu kwasasa lakini hapati ushirikiano kutoka kwa yeyote,Lakini wakati wapo ndani ya Real Madrid Ronaldo alikua anawapa moyo wachezaji ambao walikua wanapitia kipindi kigumu hivo gwiji huyo kushangaa kwanini staa huyo haoneshwi ushirikiano wowote zaidi anasemwa vibaya.kakaRonado kwasasa ambaye hana klabu baada ya kuachana na klabu yake ya zamani ya Manchester United amekua akikumbana na maneno mashambulizi kutoka kwa watu mbalimbali ikiwemo baadhi ya vyombo vya habari kitu kilichofanya magwiji kama Ricardo kujitokeza na kuona sio sahihi anachofanyiwa staa huyo.

Acha ujumbe