Beki wa Real Madrid, Rafael Varane ameripotiwa kuikubali Manchester United kuelekea msimu ujao 2021/22.
Kumekuwa na ripoti mbalimbali kuhusu uwezekano wa Varane kusajiliwa na United kwenye dirisha hili la usajili. Hii sio mara ya kwanza kwa United kuhusishwa na Varane, 2011 ilibaki sehemu ndogo kumuona Varane Old Trafford ila mambo yalibadilika baada ya kupokea simu ya Zinedine Zidane, wakati ule alikuwa mshauri wa Florentino Perez.
Miaka takribani 10, Rafael Varane amekuwa Madrid na sasa ameweka wazi kwa uongozi wa klabu hiyo kuwa anatakakupata changamoto mpya na EPL ndio sehemu anayotaka kwenda, Man United kwa msisitizo.

Japokuwa kulikuwa na ripoti kuwa United walipeleka dau la pauni milioni 50 ambalo lilikataliwa na Madrid, raisi – Florentino Perez amekanusha uhalisia wa kitendo hicho akisisitiza kuwa hawajapokea ofa yeyote inayomuhusu Varane. Japokuwa, lengo kubwa la Madrid ni kumbakiza beki huyo kwa kumpatia mkataba mpya ila kama anaweza wazi adhma ya kuondoka, huu ndio muda pekee ambao Madrid wanaweza kupata faida ya kumuuza Varane kabla hajaondoka kama mchezaji huru msimu ujao.
Changamoto kubwa inayoweza kutokea kwenye mchakato huu ni mshahara wa Varane. Inasemekana licha ya kuichagua United, Varane anataka mshahara wa pauni laki 4 kwa wiki. Huu utakuwa ni mshahara mkubwa kuliko mchezaji yeyote wa United na ni kitu ambacho Man United hawataki kurudi makosa waliyoyafanya kwa Alexis Sanchez miaka ya nyuma.


