Hearn: AJ vs Usyk Septemba 25,2021.

Baada ya pambano la Anthony Joshua (AJ) vs Tyson Fury kubuma, Eddie Hearn atangaza ujio wa pambano la lazima kwa AJ vs Oleksandr Usyk.

Fury amelazimika kuchuana na Deontay Wilder kwa mara ya 3 kabla ya kuweka mkanda wake wa WBC mezani na kupambania ubingwa wa dunia dhidi ya Anthony Joshua.

Upande wa pili, ilikuwa ni lazima AJ kuchuana na Usyk kabla ya kuweka mikanda yake mitatu [IBF, WBA na WBO] mezani na kuchuana na Fury ambapo mshindi angebeba mikanda yote minne.

Fury (kushoto) vs Wilder (kulia)

Baada ya malumbano na kulaumiana kwa muda mrefu kwa kushindwa kufanikisha pambano la AJ vs Fury, sasa ni rasmi – baada ya Fury vs Wilder (Julai 24), AJ atachuana na Usyk ambapo Hearn amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Septemba 25 pale Tottenham Hotspurs Stadium ndio tukio litakapofanyika.

Endapo Fury na AJ watashinda mapambano yao ya lazima, ni ruksa mabondia hao kupanda ulingoni na kupambania ubingwa wa dunia.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe