Richard Arnold Kutimka Man United

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Manchester Richard Arnold anaelezwa anatarajia kutimka klabuni hapo mwishoni mwa mwaka huu baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa takribani miaka miwili.

Richard Arnold anaondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwaka huu kumpisha mkurugenzi mwingine ambaye anafahamika kama Patrick Stewart ambaye atakua mkurugenzi wa muda klabuni hapo.richard arnoldTaarifa zinaeleza kua mabadiliko hayo yanafanywa na anayetarajiwa kua mwanahisa mpya klabuni hapo mmiliki wa makampuni ya INEOS Sir Jim Ratcliffe ambaye anakaribia kukamilisha ununuzi wa hisa 25% klabuni hapo.

Bosi huyo anaelezwa ana mpango wa kuifumua klabu hiyo kwenye eneo la uongozi ambalo litakwenda kuleta athari mpaka uwanjani, Kwani inaelezwa moja ya tatizo kubwa linaloikabili klabu hiyo ni uongozi.richard arnoldBaada ya kuondoka kwa Richard Arnold inaelezwa ambaye anaweza kufata ni John Murtough ambaye ndio mkurugenzi wa michezo klabuni hapo, Baada ya kuondoka kwa watu hao klabu inaelezwa kuleta watu wenye ubora mkubwa kuziba nafasi za mabosi hao ambao wameonekana kupwaya katika nafasi zao.

 

Acha ujumbe