Baada ya takribani miaka 9, Manchester United inakwenda kuanza maisha mapya bila Ed Woodward. Richard Arnold kuiongoza United.
Kabla ya msimu wa 2020/21 kuisha, iliripotiwa taarifa rasmi kutoka Man United kuwa, Woodward ataachia nafasi yake ya ukurugenzi kwenye klabu hiyo. Hii ilikuwa ni mda mfupi baada ya sakata la European Super League kuzua taharuki kwenye ulimwengu wa soka.
Hata hivyo, msimu uliisha na bado, Woodward ameendelea kuwepo kwenye nafasi yake. Japokuwa, sasa ni rasmi. Richard Arnold atakuwa Mkurugenzi mpya wa Man United kuanzia Februari 1, 2022.
Arnold anachukua nafasi ambayo haijawahi kukaliwa na mtu yeyote toka David Gill alipoiacha nafasi hiyo wakati ule ambao, Sir Alex Ferguson alistaafu kuifundisha United na soka kwa ujumla.
Uongozi wa Woodward uligubikwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosa imani ya mashabiki wa klabu hiyo. Kutokuwa na mkakati imara na endelevu kwenye idara ya kusajili wachezaji, ni miongoni mwa picha mbaya anayoiacha Woodward.
Upande wa pili, Woodward ataendelea kusifika na kuheshimika na wadau wa Man United katika upande wa kibiashara. Bila shaka, United ni timu yenye mafanikio makubwa kwenye upande wa biashara kuliko vilabu vingi vya Uingereza na barani Ulaya kwa ujumla.
Swali ni Je, Arnold atawekeza nguvu kubwa kwenye biashara au maendeleo ya soka ndani ya United? Ikumbukwe, Arnold amefanya kazi kwa karibu sana na Ed Woodward wakati wote aliokuwepo United.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.