Maambukizi ya COVID-19 yanaendelea kuwatesa watu duniani. Kwenye ulimwengu wa michezo, hiki ni kikwazo kikubwa kwa sasa.
Nchini Uingereza, takribani michezo 17 ya Ligi kuu imeshaghairishwa tokea mwanzoni mwa mwezi Disemba mpaka sasa. Na bado, huenda kukawa na muendelezo wa michezo kughairishwa kwa sababu zinazohusiana na COVID-19.
Kuelekea michezo ya hatua ya 3 ya Kombe la FA, Kocha wa Burnley, Sean Dyche na kocha wa Man City, Pep Guardiola, watakosekana viwanjani baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo.
Kwa Burnley, tayar wanamichezo 3 ambayo imeshaghairishwa mpaka sasa. City ndio timu pekee ambayo haijakumbana na dhoruba la mchezo wake kughairishwa mpaka sasa. Lakini, imeripotiwa kuwa, Man City wanajumla ya watu 21 (wachezaji na wafanyakazi) ambao wameathirika. Miongoni mwao ni Pep Gurdiola na msaidizi wake, Juanma Lillo.
Kutokana na hali ilivyo, kocha msaidizi, Rodolfo Borrell, ataiongoza Man City kwenye mchezo dhidi ya Swindon huku Sean Dyche pia akiendelea kukaa karantini na kuwakosa Huddersfield.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


