Roberto Firmino Majeruhi Kumuweka Nje Wiki Nne

Mshambuliaji wa liverpool Roberto Firmino atakosekana kwa wiki nne kwenye kikosi cha liverpool kutona na maajeruhi ya misuri.

Roberto Firmino mwenye miaka 30 ameifungia Liverpool magoli manne kwenye michezo nane ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu, Firmino alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Atletico Madrid ambao uliisha kwa Liverpool kushinda 2-0.

Roberto Firmino
Roberto Firmino

Klopp akihojiwa kuhusu kumpoteza mshambuliaji huyo alisema, “tunazungumzia majuma, bado tuna zaidi ya wiki nne, nayachukulia ni majeraha makubwa.”

Pia Klopp alizungumzia kuhusu kwaacha kiungo wake Curtis Jones na mlinzi Joe Gomez kwenye mchezo watakao  safiri kwenda jijini London kumenyena na West Ham siku ya jumapili.

“Curtis ni habari nyungine tofauti na firmino, yeye hakuwa na bahati mazoezini, yeye alipata maeraha kutokana na kidole kukwangua sehemu ya jicho, yeye yupo karibu kurudi ila itabidi tusubiri ni lini atarejea.”

“Curtis, atarudi baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa, ila baada ya michezo ya kimataifa tutaangalia ni lini anaweza kuwa sawa kucheza tena, na Joe natumai nae atarudi baada ya michezo ya kimataifa pia”

Liverpool wapo nafasi ya pili kwa sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza pointi tatu nyuma ya Chelsea najumapili wanakutana na wagonga nyundo wa London kwenye dimba la London.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe