Mchezaji lijendi na mwenye heshima kwenye historia ya Manchester United, Wayne Rooney, aweka wazi ndoto yake aliyonayo kwenye klabu hiyo.
Rooney anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa United mwenye idadi kubwa ya magoli lakini pia, anatazamwa kama mfano wa kuigwa na baadhi ya wachezaji waliopo kikosini hapo kwa sasa.
Ukimzunguzia “Wazza” unamzungumzia kocha Mkuu wa Derby County. Msimu huu hali sio shwari wakiwa wanashika mkia kwenye msimamo wa Ligi ya Championship. Pamoja na hali yao kwenye klabu hiyo, Wayne alipata nafasi ya kuzungumza na Everton lakini aliigomea, unajua kwa nini?

Akizungumza na gazeti la The Sun, Rooney amethibitisha nafasi aliyoipata (kuzungumza na Everton) lakini, aliikataa nafasi hiyo. Kukataa huko kumeambatana na azimio la Wazza ambaye pia, ameweka wazi ndoto yake ya kutaka kuwa kocha wa Manchester United hapo baadae.
Wazza anasisitiza kuwa, kila anachokifanya sasa hivi, ni maandalizi ya kuifikia ndoto hiyo ambayo kwa sasa, anaona bado hayupo tayari kukabidhiwa mikoba ya kuiongoza The Red Devils.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.


