Simba SC Inaiwaza Robo Fainali.

Klabu ya Simba SC ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa mwisho wa makundi ya Kombe la Shirikisho. Joto la kuisaka robo fainali lapanda!

Ni kawaida kwenye ulimwengu wa soka, timu zinapoelekea kwenye michezo ya maamuzi, mambo huwa ni moto!! Ni vivyo hivyo kwa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC. Wikiendi hii show nzima ipo kwa Mkapa…

Naam, dimba la Benjamin Mkapa litaamua hatma ya wanamsimbazi kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Kuelekea kwenye mchezo huo, wanamsimbazi wanashika nafasi ya 3 kwenye kundi wakiwa na alama 7 tu.

US Gendarmerie wanashikilia mkia wa kundi hilo wakiwa na alama 5 wakati ambao, RSB Berkane watachuana na ASEC Mimosas ambao waliwalaza na viatu Simba SC kwenye mchezo uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Afisa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally, amegusia vitu vichache ambavyo mashabiki wa klabu hiyo wanapaswa kuvijua na kushiriki kwa wingi.

Simba

Kuhusu hali ya kikosi: Wachezaji wa msimbazi ambao walikua timu ya Taifa, wameruhusiwa kuondoka kwenye kambi ya timu ya Taifa na tayari wameshajiunga na wenzao kwenye maandalizi ya mchezo wa wikiendi hii. Ukimtoa Hassan Dilunga, wachezaji wengine wote wapofiti kupambana kwenye mchezo huo.

Hamasa Ndani ya Uwanja: Ni desturi ya mashabiki kwa nafasi zao, kuimba nyimbo mbalimbali wanapokua uwanjani kama sehemu ya kuhamasisha na kunogesha mchezo. Safari hii, uwanja wa Benjamin Mkapa utasikika ukiburudisha kwa mfumo wake wa sauti. Unaambiwa hivi, nyimbo za Simba SC zitapigwa kwenye maspika yote ya uwanjani na mashabiki watapata nafasi ya kuimba kwa pamoja.

Jumatano Nyekundu: Mashabiki na wakereketwa wa Simba watakua na jambo lao Jumatano hii, wanamsimbazi kwa ujumla wao, watakutana pale Stendi ya Magufuli (saa 4-5 asubuhi) kwa lengo la kufurahi na kuisherehekea klabu yao. Tukio hili litahudhuriwa na Mwenyekiti wa klabu, Ndugu Murtaza Mangungu.

Unaambiwa hivi, kule msimbazi kila wanachokifanya sasa hivi ni Robo Fainali! Sio kula, kulala, kutembea, mazoezi n.k macho na akili vyote vipo Kwa Mkapa, Aprili 3, 2022.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe